Simba imeshindwa Kuifunga Toto Africans CCM Kirumba kwa Mwaka wa Saba Sasa

October 23 2016 mchezo wa round ya kwanza wa Ligi Kuu soka Tanzania bara kati ya Simba dhidi ya Toto Africans ndio Simba ilifanikiwa kupata ushindi wake kwanza wa magoli 3-0 dhidi ya Toto Africans baada ya kutopata matokeo katika mechi zao sita mfululizo wakicheza dhidi ya Toto Africans.

Leo April 15 wekundu wa Msimbazi Simba walicheza dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa CCM Kirumba huo ukiwa ni mchezo wao wa round ya pili ya Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017, Simba waliingia katika uwanja wa CCM Kirumba wakiwa na kumbukumbu ya kutopata matokeo mazuri dhidi ya Toto Africans kwa mwaka wa saba sasa.

Simba leo wakiwa katika uwanja wa CCM Kirumba wameendeleza rekodi ya kutopata matokeo chanya dhidi ya Toto Africans katika uwanja huo, Simba wamelazimishwa sare tasa (0-0) licha ya kuonesha dhamira ya kuzihitaji point tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania Ubingwa wa VPL ambao wameukosa kwa miaka minne.

Katika mechi saba zilizopita Simba ikicheza na Toto Africans imefanikiwa kushinda mara moja October 23 2017 kwa magoli 3-0, imepoteza mara mbili na sare mara nne, hivyo ukijumlisha na sare ya mchezo wa leo Simba anakuwa katoka sare dhidi ya Toto mara 5 kati ya mara nane walizokutana karibuni.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad