Simba Wataka Kufanya Maandamano ya Amani, Wamechoshwa na TFF


KUFUATIA sakata la kamati ya katiba, hadhi na wachezaji kuliweka tena mezani suala la Klabu ya Simba kupewa pointi 3 dhidi ya Kagera baada ya kumchezesha Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano, wekundu hao wa Msimbazi wametuma barua kwa Kamanda kwa kanda maalum Mkoa wa Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro kuomba maandamano ya amani. 

Maandamano hayo amb kwa mujibu wa barua hiyo ya leo yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne kuanzia majira ya saa 4 asubuhi mpaka saa 7 mchana yakianzia Makao Makuu ya klabu hiyo kuelekea  Ofisi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Dhumuni kuu la barua hiyo ni kupinga namna Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF kufanya vitendo na maamuzi ya uonevu kwa Klabu ya Simba huku malalamiko mengi ya msingi wanayopeleka maombi yakiwa hayasikilizwi kwa wakati. 

Mbali na hilo ni pamoja na leo, Shirikisho hilo kuamua kumpeleka Msemaji wa klabu hiyo Hajji Manara mbele ya kamati ya maadili ikiwa wanaonyesha nia ya kutaka kumfungia na kumziba mdomo ili asioongelee uonevu unaofanywa dhidi yao. 

Barua ya kuomba maandamano hayo ya amani imendikwa na Rais wa klabu hiyo, Evance Aveva na kutuma nakala kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) na maandamanio hayo yatapitia katika barabara za Msimbazi, Nyerere na Chang'ombe. 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad