Na kwa kuwa walisema yeye JK ni Rais dhaifu, asiyechukua hatua, anayewachekea n.k..ndipo sasa akatuletea CHUMA!....I mean "CHUMA kilichopo hapa Ikulu ya MAGOGONI muda huu,...Mirija imezibwa...Vibaka wameshikwa Koromeo...Wauza Unga wanasaga meno....Chuma kinanyoosha nchi!..wanapiga kelele kama ndama!.
JK wakati anaondoka alisema wazi "Mimi naondoka, mlisema mimi mpole, sasa nimeleta Chuma hiki"...na kana kwamba haitoshi akasema "Kila zama na kitabu chake"...akaondoka zake...Chuma kikaingia kazini.
Siku ya kwanza Kazini JPM akaanza na Management by Walking Around (MBWA)..akashusha Mbwa wakali kunusa Wizara ya Fedha....watu wakasema "anaigiza huyo!"...sasa leo 2017 igizo limekuwa Isidingo?..Mbona mnabweka?....mtulie "Bado"
Watu wakapinga hata ununuzi wa ndege kufufua ATC,.ndege zikaja wakaita "Pangaboi" akiwemo zitto ambaye akasisitiza ni "Reject" hazifai!...Wakaenda mbali kwa kusambaza picha za ndege za zamani zilizoanguka kwamba Raia watishike wasipande..lengo likaferi..halafu hao hao wanahoji eti oo hizi bilioni 8 kwa hizi ndege mbili tunaomba mchanganuo wake !...Vituko!
Wapo wanaocheka sera ya Viwanda...kwamba wanauliza viwanda viko wapi kana kwamba Viwanda ni Vyandarua vya UNICEF unasambaza...thats Means hii inaonyesha namna gani watu hawataki fedha zielekezwe kwenye miradi itakayogusa future Generation, yaani kiwanda kitakachozinduliwa 2021 hawataki...Fly Overs zitakazozinduliwa 2018 hawataki...Kiwanda cha nguo kitakachokamilika 2018 hawataki ...madaraja hawataki...wanataka vitu vianguke kama mabibo juu ya mkorosho...kwamba Viwanda wanaita ''Vi-Wonder"..just hitting their own backbones...who cares?
Most of Wanahabari wamekuwa mateja wa udaku, wanasema Uhuru unaminywa...Uhuru wa Manyani..hivi kuna mtu kawakata kuandika"MADAWA YA KULEVYA NI HATARI"on front page?..kutwa ni ku-attack personality za watu kuliko maslahi ya taifa...hawa nao wanamkumbuka JK ambaye walijisikia huru kumuandika kwa namna wanayotaka na wengine bila staha na Adabu....halafu njaa yao nayo inawafanya wanatofautiana misimamo!..leo wanasema Papai..kesho Tango...hii ni ishara ya kwamba kuna influence nyuma yao..tena inayohitaji TAKUKURU!