TATIZO la Nguvu za Kiume na Suluhisho lake

Ukweli ni kwamba ndoa nyingi za Kikristo zinavunjika kutokana na tatizo hili. Je, hakuna haja ya kuitisha mjadala wa kitaifa? Taifa letu linaangamia kwa kukosa maarifa.

Hivi upungufu wa nguvu za kiume ni nini? Kifupi ni mwanamume kutokuwa na uwezo wa kutoa mbegu bora zenye uwezo wa kutungisha mimba, au kutosimama kwa uume.

Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya wanandoa nchini wanakabiliwa tatizo hili. Kwa hiyo, mabango ya waganga yaliyopo barabarani hayajapunguza kabisa tatizo hilo.

Hawa watu wanatibu watu au majini? Hapo ndipo kiini cha makala haya. Sababu kubwa ya ongezeko la wenye matatizo haya ni kwamba dawa nyingi zinazodaiwa kuponya tatizo hili hazina viwango vya kuitwa dawa, bali ni vichocheo tu kwani kinachopigiwa chapuo huwa ni kumudu tendo kitandani na si nguvu asilia.
Waganga wengi wameelekeza nguvu zao huko na ni hapo ndipo janga hili la kitaifa linapoota mizizi.

Ukweli ni kwamba upungufu wa nguvu za kiume hauondolewi kwa dawa za kuchochea nguvu wakati wa tendo. Hizi zina madhara makubwa na mara kadhaa husababisha vifo kwa wanamume wengi wakiwa ‘guest’ na vimada wao kwani hulipua moyo.

Ni lazima kiini cha tatizo hili kichunguzwe na tiba stahiki ipatikane. Kinyume cha hapo, janga hili linaweza kugeuka na kuwa dubwana kubwa la kutumaliza.
Matatizo ya nguvu za kiume huchangiwa na kuugua kwa muda mrefu, ugonjwa wa kisukari, kuvaa nguo za kubana sana, mionzi ya simu, kompyuta na mengineyo. Pia dawa za kuua wadudu huleta tatizo hili kwani zina viambata sumu viitwavyo ‘estrogen’, matatizo ya kisaikolojia, kupiga punyeto kwa muda mrefu na kutumia vyakula vyenye kemikali.

Utafiti unasema kuna uhusiano mkubwa sana kati ya upungufu wa nguvu za kiume na kuwa na sumu mwilini zinazotokana na vyakula vyenye kemikali tunavyobugia kwa kupenda au kutokupenda.



Kuna aina 9 ya vyakula ambavyo vimefanyiwa utafiti na kubaini kuwa ni moja ya vyakula vinavyosaidia kuongeza nguvu za kiume na havina madhara katika engezeko la nguvu za kiume, katika vyakula hivyo vyenye uwezo wa kuongeza nguvu za kiume kiasili ni:

1. TANGAWIZI

- Tangawizi ni moja ya chakula kinachoweza kurejesha nguvu za kiume, unaweza kuichemsha tangawizi na ukatumia kwa kuinywa kama chai Asubuhi, mchana na jioni pia Tangawizi unaweza ukaitumia katika mchanganyiko wa kiasili kwa kutumia habat soda,asali,kitunguu saumu na tangawizi yenyewe. 

JINSI YA KUTUMIA MCHANGANYIKO HUU: 

Chukua tangawizi na kitunguu saumu vitwange kisha vichanganye na asali pamoja na unga wa habat soda na uwe unakunywa mchanganyiko huu kwa kutumia kijiko cha chai kimoja kutwa mara 3 kwa muda wa wiki moja na utaona mabadiliko.

2. TIKITI MAJI:

Chakula kingine kinachosaidia katika upande wa kuongeza nguvu za kiume ni tunda la Tikiti Maji, unaweza ukachukua tikiti lako ukalikata na kutengeneza juice ya Tikiti kisha unakunywa ila sio lazima utengeneze Juice hata lenyewe tu unaweza ukalila. Ila jitahidi kutumia tunda hili hata kila siku kwani linasaidia sana kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume.

3. UGALI WA DONA

Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake. 

4. CHUMVI YA MAWE

Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku.


5. MAJI YA KUNYWA

Kunywa maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku. Maji ni mhimu katika kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini.

6. MBEGU ZA MABOGA

Ziloweke katika maji yenye chumvi, zikaushe. Zikaange kidogo bila kuziunguza. Tafuna mbegu 100 kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja. Mbegu hizi sifa yake kubwa ni kuongeza wingi wa mbegu za kiume (manii), kama unatatizo la kuwa unatoa manii machache (low sperm count) basi hii ni mhimu sana kwako. Sasa, hizi usizitumie tu kama dawa, zitumie kama chakula na hivyo ziwepo tu nyumbani muda wote na kila siku uzitafune iwe unaumwa au hauumwi.

7. ASALI NA MDALASINI

Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 4 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila unapoenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja.

Hata baada ya mwezi mmoja kuisha bado nakushauri uendelee kuitumia asali hivi maisha yako yote au hakikisha haipiti siku bila kunywa au kula chakula chenye asali ndani yake. Unaweza kuitumia asali kila siku kwenye mkate kama mdabala wa siagi au blueband au ukaitumia kwenye juisi na kwenye chai kama mbadala wa sukari.


8. CHAI YA TANGAWIZI

Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume. Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.

Ulaji wa tangawizi mbichi nusu saa kabla ya tendo la ndoa husaidia katika kuongeza hamu na nguvu ya tendo la ndoa. Unaweza ukanywa chai ya tangawizi tu nusu saa kabla ya kuanza tendo au unaweza ukatafuna kipande cha tangawizi mbichi kwa ukubwa wa dole gumba la mtu mzima nusu saa kabla ya tendo.

Kunywa chai ya tangawizi mbichi kila siku, katika chai hiyo unayopika ndani yake weka tu maji na Tangawizi mbichi uliyosagia ndani yake (usiongeze majani ya chai humo), kumbuka tangawizi inaoshwa tu na maji na uisagie ndani ya sufuria pamoja na ganda lake la nje. Sasa badala ya kutumia sukari wewe tumia asali kwenye hii chai yako ya tangawizi na ukiitumia hivi kila siku hutachelewa kuona faida zake. Tangawizi peke yake ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini!

9. UNGA WA UDISHE

Unga wa mti wa udishe ni mzuri sana katika kutibu tatizo la nguvu za kiume na pia unasaidia sana kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume lililosababishwa na kujichua au kupiga punyeto kwani huimarisha sana mishipa ya uume. Udishe inapatikana pia katika mfumo wa juisi. Pia unaweza kuutumia hata kama unasumbuliwa na tatizo la kisukari pia unao uwezo mkubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa hata kwa kina mama.

Udishe pia unatibu magonjwa yafuatayo bila shida yoyote; Pumu, Chango la uzazi, Kupooza mwili, Unaondoa kabisa gesi tumboni na Kuongeza nuru ya macho kuona.
Udishe unao uwezo pia wa kuongeza ukubwa wa uume wako. Labda utauliza kwa namna gani?, kwa sababu moja ya kazi zake mwilini ni kuponya mwili uliokuwa umepooza, mwili unapokuwa umepooza ina maana hata damu yako pia inakuwa haitiririki vizuri kama inavyotakiwa na tuliona hapo juu kwenye somo hili umhimu wa mzunguko wa damu ulio bora katika nguzu za kiume.
Kwa kuwa mwili ulikuwa umepooza, udishe unapokuja kukutibu inakufanya kuwa mtu uliyechangamka na damu yako itaanza kuwa inatiririka kwa mtiririko mzuri zaidi na kama matokeo yake utaanza kuona hata ukubwa wa mheshimiwa unaanza kuongezeka kidogo kidogo. Na hii ni hasa kwa wale ambao walizaliwa na uume wa kawaida lakini sababu ya punyeto, lishe duni au stress walijikuta maumbile yao yanaanza kusinyaa au kupungua badala ya kuongezeka.

Na iwapo utatumia juisi ya udishe basi vitu vingine vyote hapo huhitaji kuvitumia isipokuwa ugali wa dona ambao ni lazima kila mwanaume ale na siyo ugali wa sembe ambao hauna thamani yoyote mwilini.

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nawezaje kuupata unga wa udishe??

    ReplyDelete
  2. Nawezaje kuupata unga wa udishe??

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad