TRA Yajikakamua Kufikia Malengo ya Ukusanyaji Kodi...!!!


Katika kuhakikisha mafanikio ya ukusanyaji kodi yanafanyika kwa uhakika na kuongeza pato la Taifa, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Trilioni 10.87 mpaka kufikia Machi mwaka huu kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Charles Kichere wakati wa mahojiano na Televisheni ya Taifa (TBC) katika kipindi cha Tunatekeleza.

Amesema, kuwa mwaka huu wa fedha 2016/2017 TRA inatakiwa kukusanya Trilioni 15.105 hadi kufikia Machi mwaka huu TRA imefanikiwa kukusanya Shilingi Trilioni 10.87.

Aidha, ameongeza kuwa mpaka kufikia Juni mwaka huu TRA itahakikisha inatimiza lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 15.105 ili kusaidia  Serikali kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

“Tunatumia mfumo wa Tehama kukusanya kodi na mifumo mingine mbalimbali ili kurahisisha watu kulipa kodi wakiwa nyumbani na kuepuka usumbufu,” amesema Kichere.

Hata hivyo, Kichere ameongeza kuwa kwa mwaka huu wa fedha mapato yameongezeka mpaka kufikia asilimia 9.9 hadi 10 licha ya kuwa kuna baadhi ya maeneo hawakuweza kukusanya.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad