TRA Yatangaza Kukusanya Tsh 10.87 Trilioni Kuanzia June 2016 Mpaka March 2017..!!!


Mamlaka ya Mapato Tanzania imekusanya kodi ya jumla ya Sh. Trilioni 10.87 katika kipindi cha miezi tisa ya mwaka wa fedha 2016/17 ambapo makusanyo hayo ni sawa na ukuaji wa makusanyo ya asilimia 9.99

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipa Kodi, Richard Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania inawashukuru walipakodi wote ambao wameitikia wito.

“TRA inatoa wito kwa kila mlipakodi kuwajibika kulipa kwa wakati pamoja na kufichua wale wasiotimiza wao kikamilifu,”amesema Kayombo.

Aidha, pamoja na mafanikio hayo kwa kipindi cha miezi tisa Mamlaka hiyo itaelekeza juhudi zake katika kukusanya kodi mbali mbali ili kuhakikisha lengo la mwaka la kukusanya Trilioni 15.1 linafikiwa.

Hata hivyo, amesema kuwa TRA inazidi kusisitiza matumizi mashine za EFD pamoja na zoezi la uhakiki wa TIN katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Tanga na Pwani linaendelea hivyo wananchi wanatakiwa kuhakikisha wanatumia mashine za EFD.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad