Katibu wa Bunge, Thomas Kashililah, amesema uchaguzi wa wabunge wa bunge la Afrika Mashariki(Eala) utafanyika Mei 10 mwaka huu.
Kashilila ameliambia bunge leo kuwa uteuzi wa majina ya watakaogombea uchaguzi huo utafanywa na vyama Mei 3 na uchaguzi ni Mei 10.
Chadema ilishindwa kupata wawakilishi wa wabunge wa Eala baada ya majina waliyoyapeleka, kupigiwa kura ya hapana.
Chadema kiliwateua Lawrence Masha na Ezekia Wenje kuwania ujumbe wa bunge hilo la Eala.