Uchambuzi..Hivi Ndivyo Marekani Atakavyofanikiwa Au Kushindwa Kumpiga Korea Kaskazini Katika Vita Inayonukia Huko Korea Kaskazini..!!!


Kukiwa bado tunaendelea na uchambuzi wa kile kinachoendelea eneo la Asia Pacific leo tutakijita kwenye uwezekano wa Russia na China kushiriki vita hvyo kama vikitokea je Russia na China watachagua upande gani ktk vita hvyo?

Nchi zote kabla hazijafanya maamuzi magumu ya kuingia vitani jambo la kwanza ni kutafuta waungaji mkono au watakao support ktk uvamizi huo leo US pamoja na uwezo na ubabe wake anakwenda vitani na nchi washirika ikiwamo UK na nchi zingine zinaweza kutoa mchango mwingine sio lazima mchango wa askari au vifaa inawezekana zikawa taarifa za intelligence au kuruhusu kutumika kwa airspace yako au viwanja vyako vya ndege hasa cargo plane za kijeshi kwa ajili ya usambazaji wa vifaa au huduma ndani ya uwanja wa mapambano

Nilisema linapokuja swala la Maslai ya wazungu duniani wanakuwa kitu kimoja mzungu wa SA ,Australia mpaka Canada wanakuwa kitu kimoja so tutegemee ushirikiano mkubwa kutoka Ulaya na nchi zote za wazungu watakuwa nyuma ya USA ktk jamii za wazungu Russia ndio ameamua kujitenga na wenzie na kitendo cha yeye kujitenga kimemfanya kuwa ni threat kwa wenzie(Wazungu) lakini kutokana na uwezo wake kijeshi wameshindwa kumdhibiti baada ya kifanikiwa kuangusha USSR

CHINA amekuwa mashirika mkuu wa US na Ulaya ktk nyanja mbalimbali kuanzia uchumi, biashara na uwekezaji Marekani amewekeza $228 billion ndani ya China wakati China amewekeza $64 billion ndani ya Marekani so ukiangalia Marekani amewekeza sana ndani ya China na kumfanya china kuwa mshirika mkuu ktk eneo lote la Asia lakini mahusiano ya China na Marekani yamekuwa kibiashara lakini kijeshi wamekuwa kila mtu ana mashaka na mwenzie hii imepelekea kuwa kama na bifu la kijeshi na Urafiki wa kibiashara na Uchumi

RUSSIA nchi hii imeshapitia ktk nyakati mbalimbali na US na nyakati vying US ameibuka mshindi kuanzia kuigawa USSR , Vita vya Afghanistan December 1979 to February 1989 mpaka leo NSA wanamsemo "Warusi walikuwa wepesi kuwaona wagumu kuwaua lakini magaidi ni wagumu kuwaona wepesi kuwaua" Russia na Marekani wamekuwa maadui wanaokaa meza moja ya mazungumzo na kunywa lakini ndani ya moyo kila mmoja anawaza mabaya juu ya mwenzie.

NORTH KOREA ni nchi yenye mipaka sehemu 3 mpaka wa kwanza ni mpaka wake na South Korea mpaka huu unafahamika kama DMZ Demilitarized Zone mpaka pekee ambapo US ataitumia kuingia NK kama mpaka wa kuingia kwa miguu mpaka mwingine ni mpaka na China ambao unapatikana kwenye jimbo la Jilin mpaka wenye 1,420 kilometres na unatenganishwa na mito ya Yalu na Tumen

Kaskazini mwa korea kaskazini kuna mpaka mwingine ambao ni mpaka wake na Russia mpaka mwenye 17 kilometres ardhi na 22.1Km ni maji (mto)ndio unawatenganisha sasa wote tunajua eneo la Alaska lilikuwa eneo la Russia then wakauziwa Marekani umbali wa kutoka Alaska mpaka Russia ni 53 miles sawa na 85 km sasa kitendo cha US kuingia North Korea na kuikalia kijeshi inamaana anakua anaichungulia Russia wakiwa wametenganishwa na mto tu inamaana anaweza kwenda Russia kwa kuogelea tu je Russia yuko tayali kuona jambo hilo na Putin yuko tayali kunywa vodka Moscow wakati adui anaweza kuingia Russia kwa kuogelea tu?

China ktk nchi ambazo zinajiandaa kuwa Super Power kiuchumi ni China wanasema mpaka 2050 China atakuwa Super Power kwa Upande wa kiuchumi na Uchumi unaendana na nguvu za kijeshi hili uweze kulinda Maslai yako pale adui anapoingia na ktk kujiandaa na kumpokea kijiti cha Usuper power wa kiuchumi kutoka kwa USA, China hato kuwa na amani endapo USA atakuwa anajua kinachoendelea Beijing hasa ktk maswala ya kijeshi kitendo cha US kuingia North Korea na kuweka military Base kitakuwa ni kitendo cha China kukubali kuwekewa Camera chooni au bafuni sidhani kama kuna Binadamu ambae anaweza kukubali jambo hilo

Njia pekee ya nchi zote ambazo ni Russia na China kuepuka jambo hilo ni kumsaidia North Korea aidha kwa kificho au kwa wazi kwani Silaha zinaweza kutoka Russia kupitia mpaka wao kuingia North Korea na Dunia isijue pia same to China tena China wanaweza kupeleka jeshi kabisa kwani wale so ni ngumu zungu la Texas kujua huyu ni mchina au mkorea ndani ya uwanja wa mapambano 

pia kama nilivyosema Glovbal Navigation Satellite System ( GNSS) ni technologia ya mwaka 1970 watu wanaweza kudanganya na ikaleta taarifa za uongo mfano ni kwenye Project-706 (1974-1983) Pakistan Army Corps of Engineers na Inter-Services Intelligence Pakistan intelligence waliweza kutengeneza Bomu la nuclear na Dunia walishindwa kujua kinachoendelea ndani ya jiji la Islamabad si CIA,MOSSAD AU MI6 walijua kinafanyika nini hata Adui mkubwa na jirani wa Pakistan India hakujua kinachofanyika
Islamabad

Sio kwamba Russia na China wanapenda kumsaidia ila Mazingira ya wao kuwa safe na kunywa vodka Moscow na Xinjiang Black Beer Beijing kwa amani inabidi wamsaidie North Korea kwani kuna msemo unasema "Mazingira yanaweza kuhamasisha kufanyika kwa uharifu"
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad