Nanasi ni tunda lenye vitamini mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitamin A, B na C, lakini pia tunda hili linasifika kwa kuwa na madini ya chuma (iron),calcium, manganes, copper na phosphorus.
Tunda hili husaidia kutengeneza damu na mifupa, meno pamoja na nerves na misuli.
Faida zaidi za nanasi
Husaidia kutuliza matatizo mbalimbali ya tumbo, magonjwa ya bandama, ini, homa pamoja na magonjwa ya midomo (vidonda) na magonjwa ya koo (throat).
Pia tunda hili husaidia kwa wale wenye shida ya kupoteza kumbukumbu yaani kusahausahau.
Nanasi pia husaidia kwa wenye shida ya kukosa choo , rheumatism na arthritis.
Pamoja na hayo yote pia tunda hili husaidia kuthibiti matatizo fulani ya kike ambayo husababishwa na upungufu za hormones au makosa fulani katika sehemu ya yai.