Sakata la Gwajima na jina la Daudi Bashite limeendelea kutikisa maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo Askofu (mstaafu) wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg Mdegella amefunguka na kuwataka wananchi kujikita katika shughuli za kiuchumi badala ya kupoteza muda mwingi kujadili mambo ya Daud Bashite.
Askofu Mdegella alisema hayo wakati akitoa salama za Pasaka jana katika usharika wa kanisa kuu, ambapo alidai kuwa watanzania wanapoteza muda mwingi kwa jambo hilo badala ya kushughulika na mambo ya msingi yenye tija kwa Taifa .
Alisema kwa wiki tatu watu wanajadili Bashite na Gwajima badala ya kufanya kazi kwa kuwa Gwajima na Bashite wote wametoka Mwanza hivyo wanajuana vizuri.
Alisistiza kama kuna mtu amedandia vyeti atakamatwa kwa utaratibu na kuwataka watu wengine kujikita katika kufanya kazi.