UKWELI Mchungu.. Diamond Anapowapiga Bao la Kisigino Wasanii wa Bongo..!!!


MWISHONI  mwa wiki hii, nyota wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond’, amepiga hatua nyingine baada ya kujitosa katika biashara ya uuzaji wa manukato ‘Perfume’ yakijulikana kwa jina la  Chibu Perfume.

Tayari manukato hayo yameanza kuuzwa Dar es Salaam ambapo ameeleza kuwa perfume hiyo imetengenezwa nchini Dubai, huku ikiuzwa kwa Sh 105,000 za Kitanzania.

Diamond anaonekana kuwafuata wasanii wengine mashuhuri duniani ambao wamejiingiza katika biashara ya manukato na hutumia umaarufu wa nembo zao kujipatia mapato zaidi.

Kuna wasanii mbalimbali duniani wamekuwa wakijiingiza kwenye biashara hiyo na kujitengenezea mkwanja mrefu kama Robyn Fenty ‘Rihanna’ aliyetengeneza manukato yake yanayojulikana kama Kiss by Rihanna.

Mbali na Rihanna, kuna Jay Z ambaye anashika nafasi ya pili katika orodha ya Jarida la Forbes ya wasanii wa Hip Hop wanaotengeneza mkwanja zaidi, ana perfume yake inayoitwa Gold ambayo  zinauzwa kati ya Dola za Marekani $39 hadi $70.

Lakini kuna mwana hip hop, Sean Diddy Combs ‘P. Diddy’ ambaye naye ana perfume inaitwa 3AM sambamba na Brand ya maji ya  Aquahydrate ambayo yalikuwa official water ya Manny Pac kwenye MayPac, yaliochangia kumuingizia kipato na kushika namba moja kwenye orodha ya wasanii wenye fedha nyingi miaka ya nyuma.

Yote tisa kuna Jennifer Lopez ambaye ni miongoni mwa wasanii ambao wana perfume nyingi zaidi ambapo ana Orange, Jasmine, Grapefruit, Iris, Vanilla na Musk ambapo perfume ya Glow ndiyo inamuingizia  hela ndefu zaidi baada ya kuingiza dola milioni 300 kwa kila mwaka.

Kitendo cha Diamond kuanzisha brand hiyo ni wazi amewapiga bao wasanii wengine ambao wengi hutumia umaarufu wao kwenye skendo na matokeo yake baadaye hujikuta wanaangukia kwenye dimbwi la umasikini.

Diamond amethubutu, wasanii wengine wanapaswa kuamka na kutumia umaarufu kujiimarisha katika maendeleo na kufanya vitu vyenye tija katika jamii badala ya kusubiri wanasiasa wafanye.

Inajulikana wasanii wengi kwa sasa hutumia muda mwingi kupata umaarufu kupitia vitu visivyo na tija hasa kwenye mitandao ya kijamii, lakini Diamond amewakumbusha kwamba kuna maisha baada ya ujana.

Hakuna asiyejua kuna biashara nyingi za kufanya na ukatengeneza fedha ndefu lakini wasanii wamekuwa wakiona njia pekee ya kuishi ni kujianika kwenye mitandao ya kijamii.

Diamond amewakumbusha wasanii wenzake kuwa wanahitaji kutafuta kazi ili kuendana na sera ya Rais John Magufuli ya Hapa Kazu tu.

Mkali huyo kutoka Manzese anaweza kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania ambaye amejiongeza na kuanzisha vitu tofauti tofauti ili mradi aweze kutengeneza fedha.

Mbali na manukato, hakuna asiyejua kama Diamond kwa sasa amezindua tovuti ambayo wasanii wengi wanauza nyimbo, ameingia nao mikataba ambayo ina mpa faida, kwa hapo baadaye hata asipofanya muziki anaweza kuendelea kujiingizia kipato.

Wasanii bila kujishughulisha kamwe hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio. Ni vyema wasanii wakajifunza kutoka kwa Diamond kwa kile kizuri anachokifanya hasa kwa upande wa maendeleo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad