Huu mkoa umekaa kama pweza yaani umetawanyika, kiasi kwamba hata kuichora ramani yake inakuwa ngumu kidogo ukiwa Dar barabara zote kuu zakutoka mkoani zinapita mkoa wa pwani ie kusini kuna kilwa road ambapo pwani inaanzia mbele kidogo ya kongowe, kaskazini kama sikosei pwani inagawanyika, kuanzia pale kibaha mizani mpaka kuelekea bwawani (morogoro road)yote ni mkoa wa pwani, ambapo ukifuata hii barabara ya segera pwani inaenda kupakana na mkoa wa Tanga nadhani ni daraja la kuingia mkata, ukija nyerere road pwani ni kisarawe ambapo chanika ni Dar ea salaam,
haya ukipita bagamoyo road pale mbele ya boko kuna daraja la mpaka wa Dar na Pwani, makao makuu ya mkoa ya mkoa yako kibaha. Ambapo ili mtu wa kibaha afike baadhi ya maeneo ya mkoa huu ni lazima apite katikati ya Daresalaam.
Ushauri wangu huu mkoa ungekuwa absorbed na mkoa wa Dar ukizingatia mkoa wa Dar ni miongoni mwa mikoa midogo, kutoka katikati ya mji huwezi kutembea zaidi ya kilometa arobaini utajikuta tayari uko mkoa wa pwani ila mikoa mingine unakuta wilaya hadi hadi wilaya ni takribani kilometa 200.