Ukweli Mchungu...Kapu la JPM Latoa Lulu...!!!


Akiwa kwenye kapu la Rais John Magufuli linalosubiri kupangiwa kazi nyingine, Dk Mwele Malecela, mwana wa Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela, amenyofolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kupewa ulaji. 

Wakati Dk Mwele aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Magonjwa ya Binadamu (Nimr), Dk Mwele Malecela akipata kazi katika Shirika la Afya Duniani (WHO), baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa na utawala wametofautiana kuhusu hatua za uwajibishaji zinazochukuliwa na Rais Magufuli.

Dk Mwele, aliyeteuliwa na WHO kuwa Mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika, alivuliwa ukurugenzi wa Nimr na Rais Magufuli Desemba 16, mwaka jana. Taarifa ya Ikulu haikueleza sababu ya kuondolewa, lakini hatua hiyo ilifanyika siku moja baada ya Dk Mwele kutangaza uwapo wa ugonjwa wa Zika nchini.

 Akizungumzia suala hilo kwa simu, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM), Dk Benson Bana alisema Rais Magufuli hakurupuki kutengua uteuzi wa mtendaji yeyote bali huangalia rekodi zinazoonyesha udhaifu unaosababisha waondolewe.

Hata hivyo, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Mt. Augustine, Profesa Mwesiga Baregu alisema Rais Magufuli anakiuka taratibu za uwajibishaji wa watumishi wa umma.

“Rais yuko mbali kabisa na uwajibishaji, kwa sababu una misingi na kanuni zake. Huwezi kumwajibisha tu mtu kwa matukio kwa sababu anatekeleza taaluma yake. Huenda Rais anajiona yuko sahihi kwa kila jambo, lakini haitamsaidia kupata watendaji bora wa kumsaidia,” alisema.

 Akizungumzia suala hilo, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda alisema japo kuna watendaji waliokosea, lakini kuna uwajibishaji wenye utata.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad