Lowassa yuko kimya kabisa wala hazungumzii mambo yalivyokuwa ndani ya Serikali tangu atoke kwenye Uwaziri Mkuu ambao alijiuzulu mwaka 2008. Kuna baadhi ya watu wanautafsiri ukimya wa Lowassa kama ni woga ama kukiri kwamba alishiriki kwenye "Ufisadi" wa Richmond. Lakini Lowassa alikuwa ni Waziri Mkuu na kwa kawaida Waziri Mkuu hula kiapo cha uaminifu na cha kutunza siri za Baraza la Mawaziri ambacho kipo Kisheria.
Lakini pia kwa mujibu wa Katiba yetu Ibara ya 52 ambayo inataja majukumu na mipaka ya kazi za Waziri Mkuu. Waziri Mkuu anatakiwa kufanya kazi kwa kufuata maelekezo ya Rais aliyeko Madarakani. Ukisoma pia Ibara ya 35 (i) wafanyakazi wote wa serikali wanafanya kazi kwa niaba ya Rais.
Jambo la Richmond kupewa Tenda ya kuleta Jenereta za Kufua Umeme lilianzia kwenye Baraza la Mawaziri. Lowassa kutaka jambo hilo liende mahakamani ni kwa kuwa ni kwenye mahakama ndiko kwa kuapa kiapo cha kimahakama ndipo kiapo cha kutunza Siri za Baraza la Mawaziri hutenguka.
Leo Lowassa akithubutu kusema yale waliyojadiliana kwenye Baraza la Mawaziri kuhusu Richmond atakuwa anafanya jinai inayofanana na uhaini. Kama alivyosema Nape kwamba "Hawezi kusema kila kitu" ndivyo na Lowassa naye anavyobanwa na kiapo cha uaminifu kwa Rais na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Njia Pekee ya kukivunja Kiapo cha Waziri Mkuu alichokula Lowassa ni kumpeleka Mahakamani ili huko akaseme ambayo akisema leo anaweza kushitakiwa hata kwa Kosa la Uhaini! Kiapo hicho hakiwezi kutenguliwa kwa Hoja ya Richmond kurudishwa Bungeni wala kwa Mwakyembe kujiapiza kuachia uwaziri ili apambane kwenye majadiliano Bungeni,