UKWELI Mchungu..Ukisikia Tanzania Imenyooshwa Ndio Huku..!!!


Natafakari nakosa jibu kabisa kuhusu haya maisha!!!

Kisado cha mahindi hapa Moshi kimefika 5000!!

Mvua zipo ila hazieleweki kivile.

Sukari inatengenezwa hapo TPC Moshi!! Nasikia kilo inaelekea buku tatu!!!

Michele, maharage, unga wa ngano vipo juu balaa!!

Kwa watu wanao jiajiri au kufanya Kazi za vibarua na deal za kitaa wanalalamika hawana kitu.

Lundo la wahitimu wa taaluma mbali mbali wapo mtaani bila dira wala ajira.

Wafanyakazi wa serikalini wanalalamika vibaya mno kuhusu makato jeuri ya heslb!!! 15% sio mchezo ndugu!!!

Incremental za salary kimya hadi leo na bidhaa zinazidi kwenda juu!!!!

Maisha yamekuwa ya moto kama kaa la mawe lililo kolezwa na moto wa gas.

Madaraja ya mishahara kwa wafanyakazi yamesitishwa hadi leo!

Juzi Kuna mtu kanipa story kuwa alisikia wabunge wakitetea wafanyakazi juu ya increments zao na madaraja na serikali ikaahidi kulipa!!!

Hapo kati Kuna tamko lilitoka kwa kiongozi moja akidai ni lazima mfanyakazi apitie mafunzo maalum ili kupanda cheo/ngazi ya mshahara. Leo wanadai watalipa na kupandisha madaraja. Je, ni kwa mfumo upi?

Huku mtaani wafanyakazi wanadhalilika kukopa kopa madukani huku wakitukanwa na kudharaulika!!!

Siku hizi wananchi hawana heshima hata kwa walimu ambao walikuwa wakionekana kama kioo cha jamii. Siku hizi life imekuwa tight kwa walimu wengi wanaonekana jalala kwa jamii.

Elimu bure tumeikubali lakini mabadiliko mengi yamefanyika ila mwalimu kaachwa nyuma kama koti!!!

Afadhali askari walau wanalipwa posho katikati ya mwezi hata kama ni kidogo ila inawastahi.

Ni juzi juzi tu vijana wengi ambao wameajiriwa kwenye majeshi yetu ya ulinzi wamepita mikononi mwa mwalimu. Lakini maisha yao kidogo angalau.

Juzi mwalimu moja katukanwa dukani kwa mangi akienda kopa. Ashakumu si matusi kaambiwa "nyie vipi bhana!! Mshahara wenu kiduchu mnalipwa maramoja kwa mwezi kama hedhi ya mwanamke bhana!!! Toka dukani kwangu usiniletee mkosi".!!!

Hayo ndio matusi yanayo kidhi haki ya mwalimu?!!!

Hivi watoto anao wafundisha wakisikia matusi haya watamuheshimu mwalimu?

Ndio maana elimu inashuka huku wizara ikijisifia kuwa ufaulu unapanda.

Hebu jiulize, hapo zamani daraja lilikuwa
A=81-100
B=61-80
C=41-60
D=21-40
F=00-20

Hapa elimu ilikuwa bora na wahitimu wengi waliokuwa wanafaulu kwa alama D mbili tu walikuwa active.

Siku hizi mifumo inakoroga hata walimu wenyewe ukiwauliza hawana jibu.
Alama E kwa O-level liliongezwa na haijulikani kama litadumu au!! Nimegundua kitu. Ufaulu ukiwa mbovu alama E inarudishwa!! Ukiwa mzuri Alana E inaondolewa!!!

Kinachoniumiza zaidi ni kuondoa wastani wa 30 kwa kidato cha pili na kupanga matokeo katika Division/Madaraja.

Mwaka huu kama sijakosea mtoto akipata alama D mbili eti naye kafaulu kuendelea na kidato cha tatu!!!

Hapa ni sawa na kusema. Mtoto akiwa na masomo 10 na akifaulu somo moja tu kwa alama C au D mbili kapita kuendelea na kidato cha tatu!!!

Civics- F
Geography- D
Biology- F
Kiswahili- D
English- F
Chemistry- F
Agriculture- F
History- F
Physics- F

Kwahiyo kwa matokeo haya eti kafaulu!!!!
Mtoto wa kidato cha pili!!! Kesho anakuwa mtangazaji au askari!!! Nani wa kulaumiwa akifanya matukio ya ajabu?

Huku shule tunaona vioja vingi jamani. Mtoto anakuja hajui hata kuandika vizuri. Kama huamini pitia fb uone new generation ikikoment kitu. Neno hakuna=akuna!!!
Habari=Abali.
Wengine hawajui hata kuruka space kati ya neno na neno.

Pitia pia katika tasnia ya habari utaona jinsi baadhi ya vijana watangazaji wakiharibu lugha

Haya yote ni mazao ya kuharibu mifumo ya elimu na kumgeuza mwalimu jalala la jamii!!

Serikali ni lazima iangalie kwa makini suala hili. Watu wa majeshi angalau wanaishi kwenye nyumba za serikali zenye maji na umeme.

Walimu wengi wanaishi kwenye nyumba za kupanga huku wakinunua maji na kulipia umeme.

Serikali ikumbuke 15% bila increments na kupandisha madaraja. Wafanyakazi wa serikali wanageuka watumwa wa kodi za nyumba na matumbo ya familia zao.

Kujiongeza wengi wanafanya hiyo kupitia kilimo na vijibiashara. Lakini muda wote mwalimu anatakiwa kuwa kituo chake cha Kazi. Sikuhizi wanasema hata kama huna vipindi kwa Siku hiyo ni lazima uwepo tu!!

Wakuu wenye roho mbaya wameweka daftari la kusaini asubuhi na jioni. Usipoonekana unaandikiwa mtoro wakati umehudhuria na kufundisha umefundisha.!!!!

Kitendo cha kuwalipa posho wakuu wa shule wakati hawafundishi ni kuwafanya wawe watafuta matatizo ili waonekane wazuri kwa maofisa elimu.

Ubaguzi haufai. Lipa wote sawa.

By mdau wa elimu..Mwl.Mchomvu
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Enter your comment...nimemsikia mh mmoja akitoa ufafanuzi kuwa serikali haikuahidi elimu bure bali iliahidi elimu bila malipo. sasa wadau kuna tofauti gani kati ya bila malipo na bure?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad