Mikopo tunayokopa benki hapa nchini Tanzania zina riba kubwa sana kitu ambacho hufanya watanzania wengi kutofaidika sana na mikopo hiyo. Kwani kuna benki hutoza riba zenye faida ya asilimia 18%-23%.
Watanzania tulio wengi tukishachukua mikopo hiyo hukimbilia kuninua uwanja na kuanza kujenga nyumba, kisha huishi maisha ya shida sana kwa kipindi cha miaka minne mpk mitano. Wapo wengine hukimbilia kununua gari ili waonekane hapa mjini lakini hata uwanja hawana, mikopo hiyo ya benk ina mambo sana.
Wazo la kukimbilia kujenga nyumba kwa kutumia mkopo ni kujitengenezea maisha ya dhiki sana kwani makato huwa makubwa na kufanya kila siku kukimbizana na madeni yasiyoisha. Ushauri wangu na maoni yangu kama unataka kujenga au kununua gari ni bora ujiwekee mkakati binafsi unaweza amua kila mwezi kujiwekea kiasi fulani ambacho unatumia kwaajiri ya ujenzi, utafanya hivyo bila riba wala hasara yeyote.
Mikopo ya benki ni yakuwekeza katika biashara na ili ziongeze kipato na biashara hiyo irudishe mkopo huo yenyewe bila we kuathiri mapato ya kazi yako.
Kuweka pesa kila mwezi au kila sikunkutokana na maingizo yako inawezekana, kikubwa ni uamuzi thabiti na kujiwekea malengo na kuhakikisha unayafikia malengo yako.
Huu ni ushauri na maoni yangu jinsi ninavyoona namna ya kutumia mkopo wa benk kwa faida, lakini hata kama mtu akajenga nyumba ya biashara ni sahihi lakini nyumba ya kuishi ni safi sana lakini kuna hasara kubwa ndani yake.