Wabunge Kumbana Profesa Joyce Ndalichako Kuhusu Kukaa Kimya Kwa Taarifa ya Vyeti Feki Kwa Ofisi Mmoja Mteule wa Rais


Wakati Bunge likiendelea na vikao vyake mjini Dodoma, wizara tano zinatarajiwa kujikuta kwenye wakati mgumu kwenye mijadala ya hotuba zao za bajeti kutokana matukio ya hivi karibuni.  

Wizara ambazo bajeti zake zinaweza kuibua mijadala mizito ni Wizara ya Elimu; Tamisemi; Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; Mambo ya Ndani; na Wizara ya Nishati na Madini.

Wizara ya Elimu inatarajiwa kukumbwa na mjadala kutokana na kutochukua hatua zozote tangu kuibuka kwa tuhuma za kughushi vyeti dhidi ya ofisa mmoja mteule wa Rais.

Tangu tuhuma hizo zilipoibuka, si Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) wala Wizara ya Elimu iliyozungumzia suala hilo. Wizara hiyo inaendesha uhakiki wa vyeti vya elimu kwa watumishi wa umma.

Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako, ambaye amekuwa akisisitiza uhakiki huo, amekuwa  kimya katika suala la vyeti vya ofisa huyo.

  Mijadala itakayoibuka katika Wizara ya Elimu inaweza kufanana na mijadala itakayotokea Wizara ya Tamisemi inayosimamiwana George Simbachawene inayosimamia wakuu wa mikoa na wilaya.

Hii inatokana na wakuu hao  kuwaweka ndani watendaji kwa makosa ya kinidhamu kinyume cha Sheria ya Utumishi wa Umma inayoeleza bayana mamlaka za kuchukua hatua dhidi ya watendaji.

Katika mijadala iliyoibuka awali, Mbunge wa Muheza, Adadi Rajab alishauri wakuu wa mikoa na wilaya kuelimishwa kuhusu uchukuaji hatua na matumizi ya Sheria ya Tawala za Mikoa na Wilaya.

Adadi aliyewahi kuwa kamishna wa polisi na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), alisema suala la ukamataji ni taaluma inayosomewa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad