Wadau Wajitokeza Kufagilia Agizo la JPM Kuhusu Tume ya Vyuo Vikuu Nchini..!!!


Wadau wa elimu, wamemuunga mkono Rais John Magufuli kwa kutaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutoa uhuru kwa wanafunzi kuomba chuo wanachokitaka.

Baadhi ya wanafunzi walioomba vyuo kwa mfumo wa CAS, walisema utaratibu huo haumpi uhuru muombaji aliyefaulu vizuri kwenda kusoma chuo anachokitaka, badala yake anapangiwa chochote.


Mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dadley Bahemu alisema utaratibu uliokuwa unatumiwa na TCU umepoteza ndoto za wanafunzi wengi waliopenda kusoma chuo fulani lakini wakapelekwa kwingine.

Alisema ushauri wa Rais Magufuli unajenga utaratibu mzuri wa kuwapa nafasi wanafunzi kuchagua vyuo vya kwenda bila kuzuiliwa na mamlaka yoyote.

 “Tangu nikiwa mdogo nilikuwa na ndoto ya kusoma Mlimani (UDSM), bahati nzuri nilichaguliwa. Wapo watu wengi ambao nilimaliza nao walipelekwa vyuo vingine wakati nao walipenda kuja kusoma hapa,” alisema.

  Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bodi ya TCU, Profesa Joseph Mtabaji alisema hajapata taarifa rasmi kuhusu agizo hilo la Rais Magufuli lakini watakuwa tayari kulitekeleza.

Akizungumzia uamuzi huo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Afrika cha Nelson Mandela (NM-AIST), Profesa Burton Mwamila alisema utaratibu wa wanafunzi kuchagua vyuo utavipa nafasi ya kushindana kwa ubora ili kuvutia wanafunzi.

“Ni kweli, kunapokuwa na vyuo vingi mtu anatakiwa kuwa na uhuru wa kuchagua chuo. Mwingine anapenda akaishi Mtwara, atatafuta chuo kinachopatikana huko, mwingine anataka chuo cha sayansi na teknolojia, atakuja kwetu,” alisema Profesa Mwamila.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad