Wagombea wa Chadema Washindwa Ubunge wa Afrika Mashariki..Mbowe Alia Usiku Kucha...!!!


Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamewachagua wajumbe 7 wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania huku wagombea wawili wa CHADEMA wakipigiwa kura za 'HAPANA' na hivyo kushindwa kupitishwa.

Wagombea hao wa CHADEMA ni Lawrence Masha na Ezekiel Wenje, ambao pia waliungana na wagombea wengine wote kujieleza mbele ya wabunge kabla ya zoezi la upigaji kura.
Kwa upande wa CCM, walioshinda ni 

1. Fancy Nkuhi
2. Happiness Legiko 
3. Maryam Ussi Yahya 
4. Dkt Abdullah Makame 
5. Dkt Ngwaru Maghembe 
6. Alhaj Adam Kimbisa

CUF iliyokuwa na wagombea watatu kwa ajili ya nafasi moja, aliyeshinda ni Mohamed Habib Mnyaa akiwashinda Twaha Taslima na Sonia Magogo

Awali palitokea mabishano ya kikanuni juu ya wagombea wa CHADEMA yaliyosabaishwa na chama hicho kuweka wagombea wawili pekee wakati nafasi kwa ajili ya chama hicho zikiwa mbili pia.

Baadhi ya wabunge walitaka Spika atumie utaratibu wa kuwahoji wabunge kama wnawakubali ama lah, huku wabunge wa CHADEMA wakitaka wagombea hao wapigiwe kura sawa na wengine, ambapo wapiga kura wangelazimika kupiga kura za kuwakubali wagombea hao hata kama hawawataki.

Baada ya mvutano wa takriban saa moja, Spika Job Ndugai aliamua kura zipigwe, lakini kwa kundi la wagombea wa CHADEMA akaelekeza kuwa wapiga kura wa uhuru wa kuweka alama ya 'tick' kama wanamkubali mgombea au alama ya 'X' kama hawamkubali.

"Sasa maelekezo yangu ni kwamba ukifika kwa wagombea wa Chadema weka X kama humtaki, na weka tick kama unamtaka" Alihitimisha Ndugai

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo majira ya saa 7 usiku, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe amesema haki haikutendeka ikiwa ni pamoja na ubabe kutumika na upindishwaji wa kanuni, hivyo watakwenda kuitafuta haki yao mahakamani.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa Chadema wamekosea kuweka wagombea wawili wakati kuna nafasi mbili, hiyo sio sahihi. Kwa wapiga kura pia wamekosea kwa sababu wabunge hawa wanakwenda kuwakilisha nchi na si vyama.

    ReplyDelete
  2. Wale wanawake wa Chadema walilalamika kukwa hawakutendewa haki, so wamejiunga kupiga kampeni ya kuwakataa walioteuliwa kugombea, In short Chadema ndio maana haiwezi hata kuongoza nchi kwa sababu walishindwa nini kuweka usawa wa kijinsia kwa kuwateua hata wanawake wawili na wanaume wawili ili wapigiwe kura kupata hizo nafasi mbili? Wamelikoroga walipaswa pia kulinywa..

    ReplyDelete
  3. Wale wanawake wa Chadema walilalamika kuwa hawakutendewa haki, so wamejiunga kupiga kampeni ya kuwakataa walioteuliwa kugombea, In short Chadema ndio maana haiwezi hata kuongoza nchi kwa sababu walishindwa nini kuweka usawa wa kijinsia kwa kuwateua hata wanawake wawili na wanaume wawili ili wapigiwe kura kupata hizo nafasi mbili? Wamelikoroga walipaswa kulinywa..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad