Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Simon Sirro amesema mapaka sasa watu watatu wanashikiliwa kuhusiana na tukio la kuvamiwa kwa mkutano wa mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Kinondoni siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari leo (Jumatatu) Sirro amesema shauri la kesi hiyo limekwishafunguliwa na upelelezi unaendelea ili kuwabaini waliohusika huku akitoa rai kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho wanaotoa vitisho kuwa watawafuata watu fulani ili kuwashughulikia.
“Hakuna mtu au kikundi cha watu wanaweza kuwa na mamlaka ya kuwashambulia wenzake mtu kama ana malalamiko yake anapaswa kuyapeleka mahakamani na kama ni ya jinai ayapeleke polisi lakini sio kuwavamia watu kama vile wewe upo juu ya sheria,”amesema Sirro.