WAZIRI Mwakyembe Azindua ‘Maelezo TV’ ya Idara ya Habari..!!!


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe amezindua ‘Maelezo TV’ huku akiipongeza Idara ya Habari-MAELEZO kwa ubunifu mkubwa katika kuitangaza Serikali kupitia TV hiyo.

Waziri Mwakyembe amezungumza hayo wikiendi hii, mjini Dodoma, wakati akizindua televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO.

Alisema “Napenda nichukue fursa hii kwa kuwapongeza Idara ya Habari kwa kazi nzuri mnayoifanya katika Wizara hii,nawapongeza kwa ubunifu mkubwa na leo tunazindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara hii kwa mara ya kwanza katika historia ya Wizara yetu na Idara ya Maelezo kwa ujumla”.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Dkt Hassan Abbas alisema, kuanzishwa kwa televisheni hii ya mtandaoni itasaidia kwa kiasi kikubwa Serikali katika kutangaza matamko mbalimbali.

“Sisi kama Serikali tumekuwa makini katika kuimarisha mawasiliano kati yetu na wananchi na hii televisheni ya mtandaoni itatusaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha dhima ya Serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza kazi zake,”alisema Dkt Abbas.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad