Balozi Bakari Mwapachu ametoa kauli hiyo jana wakati aliyekuwa kiongozi wa Freemasons Afrika Mashariki Sir. Andy Chande mwili wake ukichomwa katika tanuru la Wahindu lililopo Kijitonyama jijijini Dar es Salaam, ambapo majivu baadhi yatamwagwa katika ufukwe wa Coco (Coco Beach) na mengine kupelekwa India.
Mwapachu aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti la Mwananchi na alisema aliyekuwa akimshawishi kujiunga na imani hiyo inayohusishwa na mashetani ni mtu mmoja ajulikanaye kama Abdul Rajab lakini hakutolea ufafanuzi mtu huyo ni nani na ana cheo gani Freemasons.
“Haa walikuwa wengi tu si yeye (Sir Chande) ila walikuwapo akina Abdul Rajab, sikuwakubalia kwa jinsi walivyokuwa wakifikiria niwe mwanachama wa Freemasons” Mwapachu aliliambia Mwananchi.
Alipoulizwa kuhusu imani hasa ya Freemasons, Mwapachu ambaye alikuwa miongoni mwa waombolezaji waliofika katika msiba wa Sir. Andy Chande alisema kuwa haijui na hawezi kuelezea.