WAZIRI Tanzania Aeleza Alivyoshawishiwa Kujiunga Freemasons

Mwanasiasa mkongwe nchini na aliyewahi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria katika miaka ya 1995 hadi 2005 amesema kuwa aliwahi kushawishiwa na watu kadhaa ajiunge na imani ya Freemasons lakini yeye alikataa.

Balozi Bakari Mwapachu ametoa kauli hiyo jana wakati aliyekuwa kiongozi wa Freemasons Afrika Mashariki Sir. Andy Chande mwili wake ukichomwa katika tanuru la Wahindu lililopo Kijitonyama jijijini Dar es Salaam, ambapo majivu baadhi yatamwagwa katika ufukwe wa Coco (Coco Beach) na mengine kupelekwa India.

Mwapachu aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti la Mwananchi na alisema aliyekuwa akimshawishi kujiunga na imani hiyo inayohusishwa na mashetani ni mtu mmoja ajulikanaye kama Abdul Rajab lakini hakutolea ufafanuzi mtu huyo ni nani na ana cheo gani Freemasons.

“Haa walikuwa wengi tu si yeye (Sir Chande) ila walikuwapo akina Abdul Rajab, sikuwakubalia kwa jinsi walivyokuwa wakifikiria niwe mwanachama wa Freemasons” Mwapachu aliliambia Mwananchi.

Alipoulizwa kuhusu imani hasa ya Freemasons, Mwapachu ambaye alikuwa miongoni mwa waombolezaji waliofika katika msiba wa Sir. Andy Chande alisema kuwa haijui na hawezi kuelezea.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad