Wenger: Sijiuzulu Ng'oo, Wanaojiuzulu Huishia Kufa Tu..!!!


Arsene Wenger ametoa mpya na safari hii amesema haondoki kwani wanaostaafu mara nyingi hufa kwa wenye umri kama wake.

Wenger, 67, amekuwa akishutumiwa na mashabiki wa Arsenal kwa kushindwa kuipa ubingwa na sasa iko nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kufungwa mechi nne kati ya tano ilizocheza.

Kipigo cha mabao 10-2 kutoka kwa Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, ndicho kilichochochea hasira za mashabiki kutaka aondoke.

Hata hivyo, Wenger ameonyesha hajali na akasema: “Sifikirii kustaafu. Wanaojiuzulu ni makocha vijana.” Pamoja na kwamba, mkataba wa Wenger unamalizika mwishoni mwa msimu, lakini Bodi ya Arsenal inampa jeuri kocha huyo kwani imemwongezea mkataba wa miaka mwili. Alisema pia kuwa atatangaza hatma yake karibuni.

“Kwa wazee kama mimi, ukistaafu, utakufa,” aliongeza Wenger, muda mfupi kabla ya mpambano wa jana dhidi ya Manchester City. Wenger anafundisha Arsenal mwaka wa 21 sasa lakini katika miaka hiyo, hajawahi kuipa ubingwa katika miaka 13.

“Of course hata mimi inaniuma kukosa mataji,” alisema. “Nikiangalia miaka 20 kwa kweli inaumiza kuona hakuna mafanikio.

“Lakini ukiangalia klabu ya wakati huo na sasa, wakati nilipofika, wanachama walikuwa saba, lakini sasa kuna watu 700, mambo yanabadilika.”

Alisema: “Ninachukia kufungwa. Ninaelewa kuwa mashabiki wanachukia kila Arsenal inapofungwa lakini kikubwa ni kushikamana na kila mmoja na kila shabiki kuangalia timu yetu hadi mwisho wa msimu, hicho ndio cha kufanya.”     
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad