Wolper Aapa Kuacha Kunywa Pombe,Adai Zimemuharibu Vibaya..!!!!


NYOTA wa filamu nchini, Jackline Wolper, amesema yupo mbioni kuachana na unywaji wa pombe kama sehemu ya mkakati wake wa kuzuia unene uliopiga kambi kwake.

Wolper ameliambia DIMBA Jumatano kwamba, anachukizwa na unene alionao kwa sasa ambao kwa kiasi kikubwa umechangiwa na unywaji wa pombe.

Alisema, amekusudia kuanza mazoezi ya gym yatakayomsaidia kurudisha mwili wake wa wembamba ambao ulikuwa unampa mwonekano mzuri zaidi.

“Unajua mimi sikuwa mnywaji kabisa wa pombe na nilikuwa siipendi kabisa, huu mwili unaouona umesababishwa na pombe kwa sababu nikinywa ndio napata hamu zaidi ya kula chakula, kwa sasa nimeanza harakati za kuhakikisha narudisha mwili wangu wa mwanzo ambao ulinifanya nionekane vizuri zaidi ya hapa,” alisema Wolper.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad