UMEZOEA kulala na nguo nyepesi za kulalia? Au unahisi vizuri zaidi ukilala na nguo nzito laini za kulalia? Watu wengi hujifunika mashuka na wengine hujifunika mablenketi kabisa.
Katika makala haya, itakufumbua macho uanze kulala uchi/mtupu kwa kutumia hoja bora zilizochaguliwa kuelezea kwanini kulala uchi ni kuzuri kwako.
Nguo za kulalia zina gharama kubwa
Ni kiasi gani cha fedha ambazo wewe hutumia kununua pea ya nguo za kulalia? Inaweza kuwa kati ya fedha za kitanzania kati ya shilingi 20,000 na 40,000 au zaidi. Ni mara ngapi huzifua hizo nguo? Sasa fikiria ni kiasi gani cha pesa na muda unachoweza kuokoa usipovaa nguo za kulalia.
Hutengeneza uhusiano mzuri ukisaidiwa na kichocheo cha Oxytocin
Natasha Turner, daktari wa tiba asilia aliyeandika kwenye blogu ya Huff Post Canada, alifichua kwamba kulala karibu au mkiwa mmekumbatiana na mwenzi wako mkiwa uchi/watupu hufanya mwili kutoa kichocheo kiitwacho Oxytocin kinachofanya ujisikie vizuri. Hii inatokea pale kunapokuwa na mgusano wa ngozi kwa ngozi, hii inaweza kusaidia kuondoa msongo (Stress) na kushuka moyo (Depression).
Oxytocin pia inaweza kupunguza shinikizo la damu, kuimarisha tumbo na kupunguza uvimbe kwenye utumbo. Pia, utendaji wako wa tendo la ndoa pengine unaweza kuboreka.
Hupelekea usingizi mwanana
Hivi unafahamu baadhi ya matatizo ya kukosa usingizi (Insomnia) yanaambatana kutokana na tatizo la mwili kudhibiti jotoridi? Taasisi ya Usingizi ya Los Angeles inaripoti kwamba hali hii haiathiri tu mzunguko wa usingizi ila pia hukuzuia kupata usingizi mnono. Kulala uchi/mtupu husaidia katika kurekebisha jotoridi la mwili (hivyo mwili hauchemki kupita kiasi, ni vibaya kuamka umelowana jasho.
Hukufanya ubaki kijana
Kama tulivyoona hapo juu kuhusu kudhibiti jotoridi kama unahitaji usingizi mzuri, Natasha Turner anashauri kuweka mwili katika jotoridi chini ya 21°C ukiwa kitandani na njia nzuri kufanta hivyo ni kulala uchi/mtupu. Hii huruhusu vichocheo vinavyozuia uzee na Melatonin ambayo hudhibiti mzunguko wa kusinzia na kuamka kutenda kazi vizuri.
Utajihisi huru, Kulala kitandani kwako, bila kuvaa chochote inakufanya kujisikia huru.
Huhamasisha vichocheo vya furaha (kuponya)
Unapolala na nguo au kulala chini ya blanketi zito unazuia utokaji wa kichocheo cha ukuaji (Growth Hormone/HGH). Hii ina maana hutoweza kupunguza mafuta ukiwa katika usingizi au hautofaidika na ukarabati wa usiku wa mifupa, ngozi na nyama za mwili wako.
Kulala uchi/mtupu pia huthibiti kiwango cha Cortisol, zinazo dhoofisha kinga ya mwili, kupandisha shinikizo la damu na lehemu (Cholestrol), kuvuruga mpangilio wa usingizi, kupunguza hamu ya tendo la ndoa na kuongeza hamu ya sukari.
Inaimarisha kujipenda
Kama una matatizo ya kutokujiamini basi kulala uchi/mtupu kutakusaidia kujifunza kujipenda. Kwa kuanza, jizoeshe kulala bila nguo kila jioni. Baada ya muda utazoea pia baada ya muda unaweza kuwa umejifunza kuupenda muonekano wako bila nguo.
Inatunza kiafya viungo vya uzazi.
Kina dada, mnafahamu mnaweza kupunguza matatizo ya mabukizi ya fangasi kwa kulala uchi/watupu? Unaweza kupunguza kuzaliana kwa fangasi na uke wako utakushukuru kwa hilo. Vilevile wanaume wanaweza kufaidika kulala uchi/watupu kwa kuwa korodani zinakuwa katika jotoridi la kutosha na uzazi unaongezeka.
Mzunguko wa damu unakuwa bora
Hakuna kitu kibaya kama lastiki inayozuia mzunguko wa damu. Ondoa nguo zenye lastiki na utajipata uko na furaha kwa mtiririko wa damu mzuri ndani mwili wako.
Kuwa na ngozi nzuri
Unapokuwa uchi/mtupu ngozi yako inapata nafasi ya kupumua. Kama una chunusi au vipele mgongoni ni kitu cha thamani kuacha hewa ya Oxygen kufika kwenye maeneo hayo. Ngozi yako inastahili uhuru kidogo na utajisikia vizuri kwa kuiacha ngozi wazi.
Kutokuwa mvivu
Faida nyingine ya kulala uchi/mtupu ni kwamba mara baada ya kuamka unakuwa na ulazima wa kuvaa nguo kwa ajili ya siku hiyo mpya na sio kuamka na nguo zako za kulalia na kutoka nazo nje.