Afande Sele afunguka haya kuhusu Saida Karoli


Mfalme wa mashahiri bongo, Afande Sele amefunguka kwamba watanzania kuupotezea muziki wa Saida Karoli na kusapoti muziki unaokopiwa kutoka mataifa mengine ni kupoteza uhalisia wa Kitanzania. 

Afande Sele amefunguka hayo karibuni  na kusema Saida ni msanii ambaye ana uhalisia wa Tanzania na kipaji hivyo hakupaswa kupotea kwenye soko la muziki, Watanzania wanapaswa kuendelea kumshika mkono na kutomtelekeza. 

"Muziki ni kipaji na Saida anacho. Saida Karoli ni hazina kwanza ni muimbaji ambaye anaitambulisha nchi yetu kwa nyimbo za asili tofauti na wasanii wengine wote waliopo kwenye 'game'. Sijaona mtu wa kumfananisha nae lakini kwa sababu wamekuja watu wengine ndiyo wanaonekana wakifanya vizuri kuliko yeye kumbe siyo"- alisema Afande. 

Aidha Afande ameendelea kuongeza kwamba " Umri siyo tatizo katika uimbaji bali kipaji cha kweli huwa hakipotei haraka kama jinsi ambavyo Saida amekuwa kimya, hebu mpeni nafasi tena kwenye muziki huu ili akapeperushe bendera ya nchi".- Afande Sele. 

Katika hatua nyingine Afande amewaasa wasanii kudumisha upendo kitu ambacho ni silaha ambayo wao kama wakongwe ndiyo iliweza kuwasaidia katika kipindi chote walipokuwa wanafanya sanaa.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yeye Afande sele akikifanya nini wakati Saida karoli anaanza kuchuja ni Diamond peke yake ambaye alimrudisha tena kwenye soko huyo Saida karoli alikwa anajulikana afruka mashariki tu lakini sasa mpaka kwenye majukbox ya matavern wanapiga ngoma ile ya diamond kwa wimbo wa Saida Karoli kwasababu mwanamziki anayejulikana kwa TZ ni Diamond tu hata yeye mwenyewe hamna mtu anayemjuwa naona bora aanze mwenyewe kujitangaza kwasababu afande Sele anajulikana Moro tu ukifuatilia ya wenzako yako yatakushinda na naona yameshakushinda RIP in music Afande sele

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad