AGIZO la Rais Magufuli la Tanesco Kukata Umeme kwa Wadiawa Sugu Latekelezwa Kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Polisi..!!


Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)  mkoani hapa limesitisha  huduma za umeme katika  mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira (Kiwira Coal mine) na ofisi za Jeshi la Polisi mkoani hapa baada ya taasisi hizo kushindwa kulipa madeni zinazodaiwa na shirika hilo.

 Meneja wa Tanesco Mkoa Mbeya, Benedict Bahati amesema mgodi wa Kiwira unadaiwa  Sh1.3 bilioni  na Jeshi la Polisi Mkoa  wa Mbeya linadaiwa Sh700 milioni. 

Bahati amesema wamefikia hatua hiyo kwa sababu wadaiwa hao hawajaonyesha nia ya kulipa madeni yao ambayo ni ya muda mrefu na hivyo kulisababishia shirika hilo kushindwa kujiendesha kwa ufanisi.

“Taasisi za Serikali  ambazo  madeni  yake ni makubwa na mwitikio wake wa ulipaji sio mzuri, tumesitisha huduma mpaka watakapolipa madeni hayo,”amesema. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari amekiri kudaiwa deni na Tanesco pamoja na kusitishiwa huduma hiyo kwenye baadhi ya vitengo na kwamba wao kama taasisi wanadaiwa kama ilivyo kwa taasisi nyingine.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad