ARUSHA: Millioni 18 za Rambirambi za watoto wa Lucky Vicent bado zinashikiliwa na Polisi...!!!


Mapema leo Saa 9:30 Am waliripoti kituo kikuu cha polisi (Central Police) Arusha Meya wa jiji la Arusha Mh. Kalisti Lazaro , Katibu wa TAMONGSCO Kanda ya kaskazini Mh. Leonard Mao, mkuu wa shule ya Lucky Vincent ,na viongozi wengine kwa lengo la Kukabidhiwa fedha kiasi cha 18 Millioni ambayo ilikuwa rambi rambi kwa ajili ya ajali ya Lucky Vincent au kutajwa kesi inayowakabili viongozi hao na kufikishwa mahakamani viongozi hao endapo wangebainika na kosa.

Sawia na hilo nikamtafuta Meya Kalisti Lazaro kwa njia ya Simu ambapo alisema "Nimewasili central nikaambiwa turipoti ijumaa" Kalisti Lazaro

Kuhusu Fedha za rambi rambi
"Fedha zipo kwa OCD pamoja na simu yangu" Bw. Mao

Akizungumza kuhusu fedha hizo pamoja na tukio nzima la kukamatwa viongozi hao pamoja na Waandishi wa habri Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha RPC Mkumbo alisema "Bado sijui chochote kuhusu hizo fedha pamoja hatua zinazoendelea dhidi ya viongozi hao akiwemo Meya
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad