Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe ameitaka Serikali kukaa na walipakodi wakubwa kupata maoni yao namna ya kuongeza mapato ya kodi ili kuokoa kudorora kwa uchumi.
"Takwimu za Wizara ya Fedha zinaonyesha biashara 7,500 zimefungwa. Athari yake inaonekana kwani mapato ya kodi nyingi yameshuka. Kwa mwaka mzima Wizara inasema biashara 200 zimeanzishwa lakini mchango wake hauonekani," amesema Bashe.
Ametolea mfano Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambayo kodi yake imepungua kwa Sh50 bilioni huku ikipunguza wafanyakazi wake.
"Wizara ikikaa na watu hawa ikajua maitaji yao, mapato ya kodi yataongezeka na mwananchi mnyonge atapata nafuu. Kodi inalipwa na wafanyabiashara sio wanyonge," amesema.