BAADA ya Kushindwa Uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki..Masha Afunguka Haya Mazito ya Moyoni..!!!!


Kada wa Chadema, Lawrence Masha amesema hana kinyongo na wawakilishi waliochaguliwa na Bunge kuwa wabunge wa Afrika Mashariki kupitia chama hicho kwa kuwa wote wanatoka chama kimoja na Kamati Kuu ndiyo iliyowapendekeza.

Masha amesema hayo baada ya kuulizwa maoni yake kuhusiana na uchaguzi uliofanywa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambao uliwachagua wanawake wawili; Josephine Lemayan na Pamela Massay kuwa miongoni mwa wabunge tisa wataoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (Eala).

“Katika chaguzi kama zile itikadi za vyama hazihitajiki. Kilichonichekesha mara ya kwanza waliturudisha kisa tuliopendekezwa na chama ni wanaume tupu, awamu ya pili walioteuliwa ni wanawake tu,” alisema Masha.

Mwanasiasa huyo alisema Watanzania walishuhudia kilichotokea na watafanya tathmini na hata kama kuna uhasama wa kisiasa katika uchaguzi ule hapakuwa wakati wake.

“Ninasisitiza sina kinyongo na kina Pamela na Josephine bali nina furaha. Nina imani nao watawakilisha vyema Eala,” alisema Masha ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Masha ambaye aliwahi Mbunge wa Nyamagama (Mwanza) alidai kuwa CCM walicheza michezo ya kisiasa kwa kuamua kuwachagua wagombea saa chache kabla ya uchaguzi bila kusikiliza sera zao.

Akizungumzia uchaguzi huo,Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Juliana Shonza alisema ulikuwa wa huru na wa haki na watu walichaguliwa kulingana na walivyojinadi sera zao.

“Hakuna mtu aliyepangiwa kumchagua fulani.Kila mtu alipiga kura kwa mgombea anayemtaka kwa uhuru bila kushurutishwa,”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad