Kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA imetoa taarifa kuhusu Ripoti aliyokabidhiwa Rais Magufuli leo asubuhi kutoka kwa Kamati iliyopewa kazi ya uchunguzi.
Kamati imetoa taarifa kuwa kampuni ya ACACIA haijatoa taarifa kamili(sahihi) ya kiasi cha madini kilichopo kwenye makanikia yaliyoshikiliwa na kwamba amri ya kuzuia usafirishaji wa makontena yenye mchanga huo inaendelea kuwepo.
ACACIA bado haijaiona Ripoti hiyo inayosema kuwa kiasi cha madini kilichopo kwenye makontena hayo yanayoshikiliwa hadi sasa katika Bandari ya Dar es Salaam ni mara 10 ya kiasi kinachotajwa kwenye nyaraka za usafirishaji. Bado wanatafuta Ripoti kamili na ufafanuzi zaidi.
ACACIA inasisitiza kuwa huwa inatoa taarifa kamili ya kila kitu chenye thamani ya kifedha ambacho tunazalisha na huwa wanalipa kodi zote stahiki kwa kila madini yanayotakiwa kulipiwa.
Wanamalizia kwa kusema watatoa taarifa zaidi kwa wateja haraka iwezekanavyo.