Barua Nzito Kwa Bongo Fleva Wote baada ya kuondokewa na Dogo Mfaume..!!!


Mungu wangu ninakushukuru kwa siku ya leo, asante pia kwa ajili ya wasomaji wangu ambao wamekuwa wakinipa maoni na ushauri wao mwingi kuhusu safu hii. Wote tunajua kuwa wiki iliyopita, wadau wa burudani walipatwa na msiba mzito, baada ya kuondokewa na msanii Mfaume Seleman ‘Dogo Mfaume’ aliyewahi kutamba na nyimbo za Hereni, Kazi Yangu ya Dukani na nyinginezo.

Dogo Mfaume alifariki dunia kwa tati zo la uvimbe kichwani, akiacha kumbukumbu ya kuwa mmoja kati ya vijana waliofanya vizuri sana kati ka Muziki wa Kizazi Kipya, akichagua Mchiriku na Mnanda, ambako pia kulikuwa na wasanii wengine wakali kama Omari Omari na Juma Mpogo. Maneno ya mashabiki na wadau wa muziki huo wanasema ni kama wakali wa Mchiriku wameisha, baada ya wote hapo juu kuwa wameaga dunia.

Hili lilikuwa ni pigo kubwa kwa tasnia ya burudani. Kwa utamaduni wetu kama jamii, tunayo jadi ya kulia na kuzikana pamoja. Ni matarajio ya watu kuwaona waandishi wa habari wengi kati ka msiba wa mwanahabari mwenzao, kuwaona manesi na madaktari wengi kati ka mazishi ya mwanataaluma mwenzao.

Hivi ndivyo ilivyotarajiwa kati ka msiba wa Dogo Mfaume, kijana aliyefariki akiacha doa la kuwahi kuwa mtumiaji mzuri wa madawa ya kulevya kati kaharakati zake za maisha.

Lakini kwa namna ya kusikitisha sana, kulikuwa na idadi ndogo ya wasanii wa Bongo Fleva, tena hata wale wanaopiga muziki wa aina aliyokuwa akiimba ambao hivi sasa unaitwa Singeli. Nilisikiti ka sana kuona kati ka mastaa wote waliopo, ni Juma Nature, Inspekta Haroun, Suma G, Mzee Yusuf na Dullayo pekee ndiyo walionekana. 

Ingawa kuhudhuria mazishi ni hiyari ya mtu, lakini utu unatutuma tujione wakosefu tunaposhindwa kushiriki matukio kama hayo, hasa yanapowahusu watu ambao kwa namna moja au nyingine tulishiriki nao wakati wa uhai wao.

Najaribu kujiuliza, kisa ni nini? Au kwa kuwa alikuwa hatambi tena kimuziki? Matarajio ya watu wengi ilikuwa kuona wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya wakifi ka kwa wingi, lakini nilichokishuhudia mimi mwenyewe ni cha
kusikiti sha.

Ni kweli enzi zake zimekwisha, lakini wasanii wa Bongo Fleva mlipaswa mmpe heshima yake bila kujali alikufa akitoka kati ka kuishi maisha ya namna gani! Tunawaona wasanii wa Bongo Fleva kati ka mazishi ya wacheza mpira, waigizaji wa fi lamu na hata wanamuziki wa Dansi.

Kwa nini mmeamua kumsusa mwenzenu? Wale jamaa waliokuwa mateja na wakaacha ambao wameishi naye sober house Dogo Mfaume kwa muda gani kama siyo mwaka na mwezi mmoja tu.

Nyinyi je? Si mmekaa naye zaidi ya miaka mitano kwenye tasnia ya muziki! Mmeshindwa nini kuisamehe siku moja kwa ajili ya kumsindikiza mwenzenu? Yawezekana sikuwaona wengine lakini kwa umati uliokuwepo si rahisi kwa msanii kuwepo na usionekane hata kama nisingekuona basi tungesikia salamu za rambirambi kutoka Bongo Fleva, lakini na zenyewe hazikuwepo.

Bongo Fleva mmeti a aibu, mmehuzunisha, mmesikiti sha, kama mmeshindwa kuhudhuria kwenye msiba, mnategemea mtashirikiana kwenye nini? Au labda kwa kuwa hakuwa na pesa kama ilivyo kwa baadhi ya wasanii? Kati ka vitu ambavyo yatupasa kushikamana, basi ni wakati wa shida, hasa tukiwa wagonjwa na hata mauti yanapotufi ka.

Kulikuwa na ugumu gani kwa wasanii hao kwenda Chanika kumzika mwenzao na kurudi? Hatuwezi kukubali kisingizio cha umbali, kwa sababu tuliwaona kwa mamia walivyosafi ri hadi Morogoro kumsindikiza Ngwair, itakuwa Chanika, sehemu ambayo wangeweza kukodi basi aina ya Coaster? Anyway, maisha ni vile mtu unavyotaka kuyaishi, lakini hakuna faraja mtu unapata kama pale unapofi kwa na matati zo, halafu watu ulioshirikiana nao wanapokuwa wa kwanza kuonyesha masikiti ko yao. Dogo Mfaume, tangulia mshkaji, lakini hawa Bongo Fleva wenzio siyo kabisa!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad