Bosi wa shule ya Lucky Vincent kufikishwa mahakamani


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha ( RPC ), Charles Mkumbo amesema wanamshikilia mmiliki wa basi dogo aina ya Coaster ambayo ilipata ajali na kusababisha vifo kwa wanafunzi, walimu na dereva siku ya Jumamosi huko Karatu, Arusha. 

RPC Mkumbo amedai wanamshikilia mmiliki wa shule hiyo kwa kuruhusu gari yake hiyo kubeba abiria wengi zaidi kuliko uwezo wa gari 
"Siku ya tukio walikuwepo abiria 38 kwenye gari katika uchunguzi baada ya kubaini hilo tumeshachukua hatua kwa mtu aliyewezesha gari hilo kupakia hao watu, tumeshamkamata mmiliki wa gari ambaye ndiye mwenye shule hii, sasa hivi tunaendelea na uchunguzi na utakapokamilika atafikishwa mahakamani" alisema RPC wa Arusha 

Kwa mujibu wa Mkumbo anasema gari hiyo ilikuwa na kibali cha kubeba watu 30 lakini gari hiyo siku ya ajali ilikuwa na watu zaidi ya 30.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pigo la msiba alilopata mwalimu mkuu ni adhabu na funzo tosha. Wamwache aomboleze na awatunze wanafunzi waliobaki. Waadhibiwe traffic police ili funzo liwe kwa wote.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad