CHANZO Cha Vifo Vingi: Ajari ya Wanafunzi wa Arusha

Wakuu,
Kabla ya yote, natoa pole kwa familia, Ndugu na marafiki waliofikwa na msiba huu katika ajari ya Bus.

Lakini pia nitoe pongezi kwa watanzania wenzangu ambao kwa namna moja au nyingine wameshiki katika kuwatia moyo na kuwapa pole wafiwa.

Ni kweli tujuavyo kwamba ajari haiepukiki lakini kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia kuna baadhi ya ajari zinaepukika.

Kwa utafiti mdogo niliyo ufanya nimegundua baadhi ya mambo ambayo yamepelekea kutokea kwa vifo vingi vya wanafunzi hawa.

1. SEAT BELT
Kuna kila dalili Bus haikuwa na seat belts, na hata kama ilikuwepo wanafunzi hawakufunga ile mikanda. Ukiangalia mwonekano wa Bus, sehemu kubwa iliyopondeka ni sehemu ya Mbele na karibia robotatu ya Bus halijapondeka Sana. Sasa kama kila mwanafunzi angekuwa kafunga mkanda wanafunzi waliokaa siti za nyuma wengi wangepona.

Kwa sababu hakukuwa na seat belt ilipelekea wanafunzi na walimu wao wote kulushwa mbele ya gari baada ya gari kukita kwenye kolongo.

2.UZEMBE WA DEREVA
Kuna kila dalili palikuwa na uzembe. Dereva alikuwa speed kubwa na gari likamshinda kwenye kona ukizingatia na ubichi wa barabara kutokana na mvua zinazoendelea.

OMBI LANGU:
wazazi/Waalimu tuwe makini muda wote na hawa watoto wetu hasa kwenye hizi School Bus, kuna ka tabia ka kulundika watoto, unakuta seat ya watu wawili watoto wamewekwa wanne. Inapelekea watoto kushindwa kufunga mikanda.

Mungu atusaidie!

By The Tomorrow People/JF

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad