CHARLES Kitwanga Aeleza Serikali Inavyomtumia Bashite Kumhujumu Jimboni Kwake


Mbunge wa Misungwi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi katika serikali ya awamu ya tano, Charles Kitwanga ameijia juu serikali na kusema kuwa inamhujumu ili apoteze jimbo katika uchaguzi ujao kwa kuamua kutokupeleka maji jimboni kwake.

Kitwanga alisema kuwa serikali imeamua kutokupeleka maji jimboni Misungwi kwa sababu wanamuandaa mtu anayeitwa Bashite kwenda kugombea katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

Kitwanga aliyasema hayo jana bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ambapo Waziri Mhandisi Gerson Lwenge aliliomba Bunge kuidhinisha TZS bilioni 672.2 kwa ajili ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Akichangia hotuba hiyo, Kitwanga alieleza hali ngumu ya upatikanaji wa maji wanayopitia wakazi wa kijiji cha Kolomije ambapo ndipo alipozaliwa Bashite.

Kuonyesha kukerwa na serikali kupuuza kupeleka mradi wa maji jimboni humo, Kitwanga alisema kuwa atahamasisha wananchi wa Misungwi kwenda kuzima mitambo ya maji ambayo ipo katika Kijiji cha Ihelele anachodai kuwa kimesahaulika katika miradi ya maji iliyopangwa kwenye bajeti ya 2017/28.

Kitwanga alisema kuwa wakati alipokuwa waziri alikuwa anashindwa kuibana serikali lakini kwa vile sasa ni mbunge tu, basi patachimbika.

Very unfair (si haki), nazungumza kutoka moyoni mwangu, haiwezekani mradi unakwenda Tabora unatumia 600 bilioni alafu watu wangu wanakosa maji hata ya bilioni 10, alisema Kitwanga

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad