CHID Benzi Afunguka Mapya Kuhusu Dawa za Kulevya Alizokuwa Anatumia..!!!


MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Rashid Abdalah ‘Chid Benz’, amesema licha ya matumizi ya dawa za kulevya kumrudisha nyuma kimuziki, ameahidi kupambana hadi mwisho ili awe balozi bora kwa wasanii wenzake.

Chid Benz ambaye kwa sasa yupo chini ya kituo kinachopambana na matumizi ya dawa za kulevya, amesema anashukuru Mungu anaendelea vyema na ni matumaini yake atarejea katika sanaa yake na kufanya vizuri kama zamani.

Alisema kwa sasa anaona afya yake inazidi kuimarika na Watanzania wategemee mambo mazuri zaidi kutoka kwake, kwani anajiona ana mafanikio makubwa zaidi tangu aachane na matumizi ya dawa hizo.

“Kwanza namshukuru Mungu kuona afya yangu inazidi kuimarika hasa baada ya upasuaji wangu kwenda vizuri, nashukuru kuona nazidi kupata sapoti kutoka kwa wasanii na watu wangu wa karibu, najiona nipo katika hatua nyingine ya maendeleo na Watanzania wategemee mambo mazuri kutoka kwangu kwani nipo vizuri,” alisema Chidi Benz.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad