CHOZI la Zitto Kabwe Kwa Wafanyakazi, Atoa Mapendekezo Hayo

Kiiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo,  Ziito Kabwe, ameleeza  kilio chake makato ya  mifuko ya hifadhi ya jamii, pamoja na kampuni zinavyopoteza asilia 5 la pato la taifa.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo ameeleza hayo katika kuazimisha siku ya wafanyakazi Duniani.

1. Serikali ifanye marekebisho ya sheria mbalimbali za kodi zinazohusisha makampuni ya kimataifa (MNCs) ili kuzuia kumomonyoa wigo wa kodi ( Base Erosion and Profit Shifting) kunakofanywa na kampuni hizi. Hili linawezekana kwa Serikali kuchukua hatua ya kupitia mikataba ya kikodi (double taxation treaties) ambayo Tanzania iliingia na nchi nyingine duniani.

Tafiti mbalimbali katika eneo hili zinaonyesha kuwa Tanzania hupoteza 5% ya Pato la Taifa kutokana na vitendo vya kampuni kubwa kukwepa kodi kwa kutumia mbinu za kihasibu (tax planning measures). Serikali yetu inapaswa kushirikiana na Serikali nyengine za nchi mbalimbali duniani katika kampeni ya kimataifa ya haki za kodi (International Tax Justice Movement).

Vyama vya Wafanyakazi nchini vinapaswa kuwa mbele kuishinikiza Serikali kushiriki kwenye kampeni hizi na pia kufanya mabadiliko makubwa kwenye sheria zetu za kodi ili kulinda wigo wetu wa kodi.

2. Serikali itazame upya michango ya wafanyakazi kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Viwango vya michango Kwa Tanzania vipo juu mno na vinapunguza kipato cha mfanyakazi na kuongeza gharama kwa waajiri. Michango ya Hifadhi ya Jamii ishushwe mpaka jumla ya 12% ya mshahara; kwa Waajiri kuchangia 7% na Wafanyakazi kuchangia 5% ya mishahara yao.

Hii itasaidia kupunguza gharama za kuajiri kwa Waajiri. Vile vile Tozo ya mafunzo SDL ishushwe mpaka 3% . Eneo hili ni muhimu liangaliwe kwa muktadha wa kukuza ajira nchini hivyo ajira zinapoongezeka mapato kwenye maeneo haya yanaongezeka pia.

3. Serikali idhibiti mfumuko wa bei kuhakikisha inapunguza gharama za maisha kwa wafanyakazi. Katika wakati kama huu ambao bei za vyakula zimepanda zaidi ya mara 2 kipato cha wafanyakazi wengi nchini kimebaki palepale, hali hii inaongeza ugumu wa maisha kwao. Ni muhimu Serikali kuchukua hatua mahsusi kudhibiti mfumuko wa bei za vyakula nchini.

Mwisho, Wafanyakazi wa Tanzania, nawakumbusha kuwa kuna mahusiano chanya kati ya maslahi yenu na aina ya uongozi wa kisiasa uliopo kwenye nchi. Msikae pembeni kwenye harakati za mabadiliko ya kisiasa nchini. Vyama vya Wafanyakazi vina nguvu zaidi ya kuhamasisha na kuweka mazingira mazuri ya kidemokrasia na utawala wa kikatiba nchini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad