DOGO Janja Afunguka Siri ya Kutupia 'Pamba' Kali..!!!


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Abdulaziz Chande ‘Dogo Janja’, amewaangalia wanamuziki wenzake wote na kubaini hakuna anayemgusa kwa kupiga pamba.

Dogo Janja amesema kwamba, moja ya siri ya mafanikio yake ni kuvaa kwani hali hiyo imekuwa ikumuongezea ushawishi mkubwa kwa jamii inayomzunguka.

Alisema amekuwa akitumia gharama kubwa kujiweka nadhifu na hajutii gharama anazotumia kwa kuwa ameendelea kuwafunika wasanii wenzake kwa upande wa mavazi.

“Unajua moja ya mafanikio niliyonayo kwenye muziki ni pamoja na upigaji wangu wa pamba ambao umekuwa ukinigharimu pesa nyingi, lakini sijawahi kujutia kwa sababu nimewafunika wasanii wenzangu wote,” alisema Dogo Janja.

Aidha, msanii huyo kwa sasa ameingia kwenye ushindani na msanii mwenzake, Juma Jux ambaye ni miongoni mwa wasanii wanaodaiwa kutupia pamba kali zaidi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad