Edo Kumwembe ' Simba inahitaji wanaume watatu wa nguvu'



Edo Kumwembe afunguka haya:

Makala ambayo msemaji wa Simba kasema ni mbovu...shabiki wa Simba uisome hapa na utafakari akili za msemaji wako

.

JICHO LA MWEWE: Simba inahitaji wanaume watatu wa nguvu
By EDO KUMWEMBE

TUKUTANE uwanja wa ndege. Simba itakuwa inasafiri labda kwenda Rwanda, Yanga itakuwa inasafiri kwenda Misri. Kule kwa Yanga kiasi wametimia, huku kwa Simba kunahitajika wanaume watatu wengine kabla ya kupanda ndege kwenda hiyo safari yao.

Simba inahitaji kuingia sokoni kwa umakini na kununua wachezaji watatu wa kigeni wa maana ambao, kwa hapa nchini sijawaona mpaka sasa. Mgongo wa timu ni mlinzi wa kati kiongozi mwenye uzoefu.

Kisha kiungo mahiri mwenye nguvu na uzoefu, halafu mshambuliaji wa nguvu anayeweza kufunga mabao 20 ya msimu.

Kwa kuanzia katika ushambuliaji Simba wamekwenda kwa John Bocco. Siyo mbaya. Kwa kulinganisha washambuliaji ambao wanao sasa hivi, Bocco ni bora zaidi. Bocco aliye fiti bila ya majeraha ni bora kuliko Laudit Mavugo au shujaa wa juzi, Fredric Blagnon.

Anahitajika mtu kama Donald Ngoma wa Yanga. Mtu msumbufu, mwenye nguvu, asiyeogopa, lakini cha msingi zaidi awe na jicho la kuona lango. Niliandika mitandaoni, Ngoma hajaichezea Yanga katika Ligi tangu Januari, lakini Mavugo hakuweza kufikia mabao yake katika ligi.

Kwa muda mrefu Simba imekosa mshambuliaji tishio huku ikishindwa kufanya vyema katika soko la uhamisho la wachezaji wa kimataifa. Tangu alipoachwa huru Amiss Tambwe na kununua Dan Sserunkuma, Simba haijapata mtu wa uhakika pale mbele.

Katika nafasi ya ulinzi Simba wanahitaji mtu kiongozi, mbabe, mwenye akili ya mpira kama Serge Paschal Wawa. Huyu Method Mwanjali inaonekana umri umesogea na ndiyo maana hata majeraha yake yamechukua muda mrefu.

Hata kama angekuwa fiti, katika mechi za kimataifa Simba tayari ilikuwa inahitaji beki wa nguvu wa kucheza naye sambamba. Juzi James Kotei amecheza vizuri katika nafasi hiyo, lakini nadhani bado anahitajika mlinzi wa nguvu zaidi.

Simba pia wanahitaji kiungo mwingine mwenye mamlaka uwanjani. Kiungo ambaye pia atakuwa kama kiongozi wa eneo hilo. Kuna utoto mwingi katika eneo la kiungo la Simba hasa
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Manara yupo sahihi, hii makala ni mbofu-mbofu, huko kwa yanga ulikosema wametimia, wamefanya nini kikubwa cha kusifiwa kimataifa?? Ebu wacha-unazi Edo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad