EVERTON Yaja Kuzifunda Simba, Yanga Julai..!!!


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe, amesema kikosi cha Everton FC kitatua nchini Julai mwaka huu kukipiga dhidi ya Simba au Yanga katika mechi maalum zilizoandaliwa na serikali ili kutangaza vivutio vya utalii nchini.

Mwakyembe alisema uongozi wa timu hiyo inayoshika nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL) ikiwa na pointi 58 baada ya mechi 35, umeweka sharti kwamba utacheza dhidi ya timu itakayoibuka mshindi katika mechi maalum ya kirafiki kati ya Simba na Yanga.

Waziri huyo aliyasema hayo bungeni mjini hapa jana alipowasilisha hotuba yake kuhusu utekelezaji wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka huu wa fedha na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha.

Alisema ili kuimarisha michezo na kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, mwaka ujao wa fedha wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, itahakikisha inawasiliana na Balozi zilizopo Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Uholanzi, Ubelgiji, Urusi, China, Japan, Jamhuri ya Korea, Canada na Marekani kwa lengo la kuzikaribisha klabu kubwa za soka za nchi hizo kuja nchini.

"Tayari tuna uzoefu wa ziara ya wachezaji wa kimataifa wastaafu wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid ya Hispania ambao walicheza na wachezaji wastaafu wa timu yetu ya Taifa jijini Dar es Salaam mwaka 2014 na kupata fursa ya kutembelea vivutio vyetu vya utalii," alisema.

"Ziara ya timu hiyo ilitangazwa dunia nzima kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na CNN, BBC na Supersport.

Alisema ujumbe wa timu hiyo tayari umeshakuja Tanzania mara mbili ndani ya mwaka huu, mara ya kwanza kujadiliana na wizara na kukagua Uwanja wa Taifa na miundombinu yake na mara ya pili kujiridhisha kuhusu ubora wa nyasi za uwanja huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad