Mchaichai ni mmea ambao unatambulika hapa nchini pamoja na Afrika kwa ujumla wake, lakini hapa nchini wengi huutambua mmea huu kama kiungo katika chai na husaidia kinywaji hicho kuwa na harufu mwanana zaidi na kuwavutia watumiaji.
Miongoni mwa faida za mchaichai ni pamoja na hizi zifuatazo:-
1. Kuzuia kutapika
2. Kutuliza maumivu ya tumbo
3. Kupunguza makali ya homa.
4. Msaada kwa wenye tatizo la baridi yabisi,
5. Husaidia kusafisha figo
6. Huzuia tatizo la tumbo kuunguruma
7. Husaidia uyeyushaji wa chakula
8. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na maumivu mbalimbali ya mwilini.
9. Husaidia kupunguza maumivu kwa kinamama wakati wa hedhi