Mara nyingi tumekuwa tukipata shida juu ya kusafisha pasi zetu za umeme punde tu inapokuwa imeanza kiushika uchafu.
Pasi za umeme huchafuka kutokana na moto kuwa mwingi, kitendo kinachopelekea nguo, hasa za mpira, kunga’ang’ania na kuharibu pasi kwa kuifanya iwe ina mabaki ya nguo yaliosababishwa na moto wa pasi ya kunyooshea kuwa mkubwa.
Tumesikia na pengine tumeshuhudia tukitumia steel wire, (dodoki la kusugulia sufuria), kusafishia pasi zetu tukiamini ni njia nzuri au kutumia kidonge cha panadol kusugulia pasi ili iwe safi. Huenda ikawa ni sahihi kwa wakati huo.
Leo nitakupatia njia rahisi za kuweza kusafisha pasi yako kwa kutumia vitu ambavyo ni rahisi, na vyepesi kuvipata, huku hata vingine vikipatikana nyumbani.
Chumvi:- Hii hutumika kama kiungo cha mboga hapo nyumbani lakini huleta matokeo mazuri ukitumia kusafisha pasi.
Jinsi ya kutumia chumvi;
Weka kiasi cha chumvi kuanzia kijiko kimoja cha chakula, kisha washa pasi yako na uwe unanyoosha pale ulipo weka chumvi, mpaka uchafu utoke. Ni kitendo kisicho zidi dakika 20.
Dawa ya meno:-Pakaa dawa ya meno yoyote kwenye pasi yako, kisha washa pasi, hakikisha pembeni kuna kitambaa chenye maji maji maana kitatumika kufuta pasi ikiwa kama njia ya kusafisha pasi hiyo.
Vinegar:- Hii hutumika kuweka katika kachumbari au salad. Chukua kitambaa kisha kimwagie vinegar na uwashe pasi mpaka ipate moto, kisha tumia kitambaa chenye maji maji ya vinegar kusafishia pasi yako.
Hakikisha pasi inasafishwa ikiwa na moto ili iweze kusafishika vizuri.