FAHAMU Mambo 15 ya Kushangaza Usiyoyajua Kuhusu Mbwa Mwitu..!!!


1. Maisha yao ni mpela mpela, hakunaga muda wa kupumzika muda wa kazi kila kitu ni mchaka mchaka tuu, wanaharaka pasina mfano.

2. Wanaamini katika sera ya kiujamaa.

3. Ni marufuku kujipaka damu wakati wa kula, na atayepatikana na damu wenzie humtafuna pia.

4. Wanapokula hunyofoa nyama hula, hujifuta damu kisha hufata nyama tena.

5. Wanaokula hutenga chakula cha
watoto, sasa wewe na ukubwa wako jaribu kula utakoma.

6. Ukimpiga mmoja akakimbia dakika tano nyingi atarudi na kundi na utajuta kuzaliwa, 
Nyati huwa wanaelewa sana kinachowapata kwa sababu ya ubabe wao.

7. Hawa majamaa huwa hawakubali kushindwa, na kushindwa kwao ni kurudi nyuma kujipanga.

8. Hutambua wanyama wagonjwa na hutumia sana fursa hiyo kuwakamata hasa wale wakubwa kama nyati na twiga.

9. Ukiwaonyesha damu ni kama umewaharibu akili hapo hawatajali wewe ni nani, binadamu, simba , chui, nyati ukianguka ndio wanaridhika.

10. Ni wanyama ambao hutumia muda mfupi sana kuridhishana kimapenzi, dakika chache tuu Biashara imeisha na kibendi juu.

11. Huwaficha watoto wao wasiwaone wawapo katika mahaba, cha ajabu watoto wao mwaka mmoja tuu nao huanza kufanya waliyokuwa wamefichwa sasa sijui wanajifunzia ndotoni.  


12. Staili wanayotumia kula hata wanyama wanaokula nyama huishia kuwatizama tuu, na hakuna anayeweza kuwasogelea hata kama ana njaa, fisi huwa anachekaa weeee mpaka anaamua akafanye kazi nyingine.

13.Wakishiba muda wao mwingi hutumia katika michezo, mfano kupigana , kukimbizana nk.

14. Kachezee chochote alichonacho Ila ukitaka ubaya naye kaguse watoto wake na kama kamoja kambeya kapige kelele, jicho utalopigwa litasadifu unachokwenda kufanywa.

15. Jike hupandwa na dume mbabe, hivyo wanyonge wa mwisho huenda kutafuta majike katika koo zingine na huo huweza kuwawinda mwanzo wa kuanzisha jamii yao mpyaa.

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Picha yako ulioiweka hapo juu siyo ya mbwa mwitu unhadithia kuhusu mbwa mwitu halafu unaweka picha ya mnyama mwingine mnazingua kweli kweli bongo suala la shule kazi ipo kwelikweli yaani bado na vyeti vyenu "fake"

    ReplyDelete
  2. Picha yako ulioiweka hapo juu siyo ya mbwa mwitu unhadithia kuhusu mbwa mwitu halafu unaweka picha ya mnyama mwingine mnazingua kweli kweli bongo suala la shule kazi ipo kwelikweli yaani bado na vyeti vyenu "fake"

    ReplyDelete
  3. Mbwa wa polisi siyo mbegu ya mbwa mwitu mdau kisheria hairuhusiwi kumfuga mbwa mwitu jina lake tayari linajielezea lenyewe"mbwa mwitu"mara nyingi mbwa wa police ni uzao mwingine kabisa hauusiani kabisa na uzao wa mbwa mwitu inaonyesha ni jinsi gani watu hatuwafahamu kabisa au uelewa ni mdogo sana kuhusu hawa wanyama wa porini japo wapo wengi kwenye hifadhi mbali mbali Tanzania ingekuwa ni wazo zuri kama kwenye moja ya TV zetu za Tanzania ikawa inakuja japo mara moja kwa mwezi documentary film za wanyama pori wa aina tofauti ili wananchi waweze kuwaelewa kuwafahamu na kuwaona live kwenye TV zetu katika mazingira yao yaxkila siku porini naamini ingetusaidia sana na sisi kuwafahamu kwani watu wanasafiri toka mbali sehemu tofauti duniani kuja kutalii kwetu ili kuwaona hao wanyama waishio nchini kwetu wakati sisi wengi wetu hasa tuishio mijini hatuwafahamu hata kidogo hilo ni wazo tu lingetusaidia sana ingekuwa ni bonge la enjoyment na wakati huo huo tunajifunza na kuwafahamu vizuri wanyama waishio nchini kwetu Tanzania

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad