MIAKA ya nyuma piga hesabu kama 50, hizi kelele zinazohusiana na wanaume kukosa nguvu za kiume lilikuwa ni tatizo linalosikika kwa wanaume wanaoanza kugusa miaka 60 na kuendelea.
Hakukuwa na shida hii kwa vijana, heshima ilikuwepo na hakuna mama aliyelalamikia tatizo hili kama ilivyokuwa miaka ya hivi karibuni ambapo kelele za matatizo kama hayo zimeendelea kusambaa kila kona.
Tatizo hili sasa linasikika kwa vijana wenye umri hata wa miaka 25 na kuendelea, labda ndiyo maana limekuwa ni janga sugu linalotishia ustawi wa jamii.
Sababu nyingi zimekuwa zikitajwa zikiwemo za nyakula, changamoto za maisha na mambo mengi, lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda inaonyesha kuongezeka kwa tatizo hili badala ya kupungua.
Habari kama hizo ni nyingi kwa namna tofauti tofauti na kwa watu wengi sana. Ni utitiri wa watu, vijana kwa wazee na vijana ndio wameshika usukani wakiongoza makundi mengine katika jamii.
Kwa bahati nzuri matatizo mengi ya nguvu za kiume yanatibika, lakini iwapo tu kama matibabu sahihi yanayoanzia kwenye chanzo cha tatizo yatapatikana na pia kujua maendeleo ya muhusika baada ya mtu kuugua hadi kupona.
Hata hivyo, kwa bahati mbaya sana waathirika wengi wamekuwa wakikurupuka tu kubugia dawa na hii ndiyo sababu wamekuwa hawaponi licha ya kutumia kiasi kikubwa na pia wamekuwa wakipoteza fedha nyingi bure tu kwa matibabu hayo.
Pia kutokana na tatizo hili kuwa kubwa, kila kukicha utafutaji wa suluhu ya matatizo haya huendelea kujitokeza, kiasi cha kutia wasiwasi.
Lakini kinachokata maini zaidi ni kwamba, wengi wa wataalamu siku hizi hawajui sababu za kupungua nguvu za kiume wala hawajui utendaji wa mwili wa binadamu. Wengi wanadhani kuishiwa au kupungua nguvu za kiume ndiyo ugonjwa wenyewe.
Kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa. Kuna sababu zake ndani ya mwili. Sababu hizo ni nyingi mno, ni zaidi ya 200! Anatakiwa daktari mtaalamu aliyebobea katika uzazi, mifumo ya mkojo, anayelijua vizuri figo ndani na nje, ini na mifumo mingine ya mwili, ikiwa ni pamoja na kemia ya mwili. Na inatakiwa dawa iende kutibu chanzo cha tatizo.
Mtu aelewe ya kwamba, anapojitibu mapema anakuwa anajitengenezea fursa pana ya kupona, kwa sababu ubaya wa tatizo hili, kadiri siku zinavyokwenda ndivyo pia ugumu wa matibabu unavyokuwa mkubwa zaidi, viungo vilivyoathirika vinakuwa vikorofi zaidi kuitika dawa kutokana na ugonjwa kuwa sugu.