GAMBO Azungumzia Siasa Tukio la Ajali ya Basi la Wanafunzi wa Lucky Vincent..!!!


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kuwa tukio la msiba wa wanafunzi wa Lucky Vincent uliotokea hivi karibuni halikutegemewa na halipaswi kutumika kujinufaisha kisiasa, huku Meya wa Jiji la Arusha akiendelea kushikiliwa na polisi.

Meya huyo, Kalist Lazaro; viongozi wa dini na baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Wamiliki wa Shule Binafsi Kanda ya Kaskazini (Tamongsco) wanashikiliwa na polisi baada ya juzi kukamatwa walipokwenda kutoa rambirambi katika shule hiyo.

Akipokea rambirambi kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwamo taasisi ya Wezesha Sasa walitoa Sh4.4 milioni, Umoja wa Wauza Mafuta Rejareja (Tapsoa) na Shule ya Dar es Salaam Independent (DIS), Gambo alisema jana kuwa kila mchango uliopokelewa utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na hakuna pesa itakayopotea.

“Tusiangalie waliofiwa tu lakini tunapaswa tuangalie na hawa wanafunzi watatu walionusurika Mungu ana mipango nao na lazima tufanye jambo kwao kwa sababu nao ni sehemu ya waliohusika katika ajali iliyopoteza maisha ya watu 35,” alisema.

Alisema kelele zinaendelea juu ya matumizi yasiyo sahihi ya fedha zote zilizochangwa hazina msingi kwa sababu wakati kuna watu waliahidi, lakini hawakutoa kwa wakati na shughuli zisingeweza kusimama na Serikali ilitumia busara kutafuta fedha ili shughuli za kusafirisha miili na mazishi inafanikiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad