Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel imetoa ufafanuzi kuhusu madai ya kuhujumu uchumi na kutoa kueleza kuwa iliingia kwenye kesi hiyo kutokana na mteja wake kuwa mhusika mkuu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Le Van Dai ameeleza kuwa makosa pekee ambayo wamehusishwa nayo na kukiri, ni kushindwa kutoa taarifa za usajili wa kampuni ya Unex Company Ltd kwa ajili ya kusajili laini za simu 1000 zilizouzwa kwa kampuni hiyo.
Kosa lingine ni kushindwa kitimiza majukumu yao vizuri kwa kuuza laini za simu kwa kampuni hiyo ambayo haikuwa haikuwa imesajiliwa kikamilifu.
Inadaiwa kuwa bila kupata kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kampuni ya Unex Company Ltd ilisimika mitambo iliyowezesha laini hizo kutumika kwa mawasiliano ya nchi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh459 milioni.
Siku zote tunafanya kazi kwa kufuata taratibu za nchi. Mitambo ambayo ilikuwa inafanya kazi ya kuiba mawasiliano sio yetu na hatukufahamu kama wateja wetu Unex walitumia mitambo hiyo,"amesema