HIVI Ndivyo Jinsi Siasa za Matukio zinavyozorotesha Upatikanaji wa Ben Saanane

Kama tujuavyo Beni amepotea sasa ni takribani miezi sita haifahamiki ni upi mustakabali wake na kinachosikitisha si tu vyombo vya dola kutokupata majibu kwa haraka,ama raia wenye mapenzi mema bali hata viongozi wa chama ambacho Beni alikiwa ni miongoni mwa kiongozi mwenzeo wanalifuatilia jambo hili kwa mtindo wa siasa za matukio.

Ndugu wanachadema mchezo wa kuwa busy kwenye siasa za matukio kunasababisha sakata la Beni kusahaulika kila itokeapo agenda mpya ionekanayo kama mtaji wa kisiasa.

Nafahamu mtasema kwamba CDM sio chombo cha Dola ila ifahamike sakata la Roma ni kama hili la beni lakini nadiriki kusema wasanii wameonesha mfano mzuri kuliko CDM kwani walisimama imara mpaka Roma akapatikana.

Juzi sakata hili lilionesha kufufuliwa na wanasiasa kama ZZK,Lissu na Mbowe lakini inasikitisha jambo hili kusahaulika kwa kuibuka isue ya Bashite.

Hivi ni sawa kuhangaika na kutumia nguvu kubwa kwa isue ya Bashite kuliko mustabali wa wapi alipo Beni Saanane?

Siku chache hapo nyuma kila mtu ni lazima kila aandikapo aweke#Tunamtaka Beni saanane akiwa hai,lakini kwa sasa watu wameshasahau kabisa.

Ni lazima CDM wakajifunza kupendana si tu wakati wa siasa bali hata wakati wa matatizo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad