HOJA Chonganishi: Star TV Ifungiwe Mara Moja,Imemdhalilisha Bashite..!!!


Kitendo cha Star TV kurusha matangazo ya mahojiano yenye mvurugano hakivumiliki. Mahojiano yasiyo na uwiano yalilenga kudhalilisha. Yalilenga kumuanika na kumfanya kuaibika RC wa Dar, Daudi Albert Bashite aka Paul Makonda.

Mahojiano yamemuacha Bashite peupe na akiwa amesawajika kiuhakika. Ubovu wa majibu; kukosa umakini na kubabaikababaika kwa Bashite kumemuacha Bashite katika hadhara ya hasara. Mahojiano yamekuwa ugonjwa wa jino. Maumivu makali kama kabali.

TCRA fungieni Star TV na wanyang'anyeni leseni. Ni katika kumlindia heshima Bashite. Mahojiano yamekoleza manjano kwenye tuhuma. Tuhuma za kubuma katika kusoma. Mahojiano yalipaswa kupangwa na kupangika kiuhakika. Si vile. Hayakufaa.

Nafasi haikutumika,nanasi limeharibika. Majivuno yameleta miguno ya kukataa kuambiwa uongo hata kwa hongo. Bashite ameumbuka. Bashite amedhalilishwa. Nani aliwatuma Star TV?

Rambirambi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Songea,Ruvuma)

Chanzo Jf

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad