Hotuba ya Prof. Jay Bungeni Yamkuna Darassa


Rapa Darasaa CMG amempongeza Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Prof Jay’ kwa kuendelea kupaza sauti Bungeni kudai maslaHi ya wasanii na sanaa yao.

 

Mbunge huyo wa Mikumi (Prof Jay) alitumia zaidi ya dakika nane Bungeni kuchangia katika bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, alichokizungumza hiki hapa chini, kisha pongezi za Darassa.


Prof Jay akiwa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Mr Two Sugu’ bungeni

Mh Spika kabla sijaanza kuchangia na declare interest mimi ni mwanamuziki  bora wa Hipo Hop Afrika Mashariki na Kati  na kusini mwa jangwa la sahara, kwa hii wizara inanihusu sana. Mh. Spika

historia ya nchi yetu inaonyesha tangu wa wahasisi wa nchi walipokuwa wanafanya harati kadha wakadha walikuwa wanatumia  sana sanaa, nakumbuka Mwl Nyerere  alikuwa akitumia wasanii mbali mbali kama Mzee Mwinamila,  Mzee Moresi Nyunyusa ambao hadi leo midundo yao inatumika katika taarifa za habari huko TBC  wakati wanafanya harakati za kupromote vijiji vya ujamaa.

Lakini Mh. Spika pia wanakina Mzee Mkapa walikuwa wanawatumia wanamashairi kama wakina Mzee Tambalizeni na watu wengine kama hao,  inaonesha ni jinsi gani sana ni kitu cha muhimu na ni nyenzo muhimu sana katika taifa  kuonyesha utamaduni, mila, lakini pia kufikisha ujumbe.

Tunajua kwamba sanaa inatumia sana mafundisho  lakini pia inakanya, inaonya  na inasifia inapobidi lakini kwa sasa kwa siku za usoni imeonekana wasanii kadhaa wakadha wamekuwa wakibanwa kutoa yale mawazo yao kama ilivyotokea kwa msanii  Roma ambaye ametekwa na akaja kuachiwa katika mazingira ya kutatanisha. Lakini pia msanii Nay wa Mitego ambaye alishikwa na baadae akaja kutolewa  kwa msamaha wa Rais, hii inawapa hofu wasanii kutoa kile ambacho walikuwa wanakifikiria kwa sababu tunaamini msanii yuko huru  na anatakiwa kutoa mawazo huru kulisaidia taifa letu.

Hata sisi tulikuwa tukifanya muziki tunaimba nyimbo kama ‘Ndio Mzee’ na vitu vingine wengi mnazijua, Mh. Waziri (Mwakyembe) wewe ulisema ni shabiki wangu  mkubwa kwa hiyo tunaamini kabisa mlikuwa mnajua jinsi tumetumia sanaa hii kufundisha kukanya , kuonya na kuburudisha pia.

Lakini Mh. Spika wasanii wa Tanzania tumekuwa tukiwatumia katika kampeni mbalimbali  kama Maleria,  na hata katika uchaguzi uliopita  mmeona jinsi wasanii walivyokuwa wakitumika,  na baadae mmewatumia kama makarai na kuwaweka uvunguni, makarani yanatumika katika kujenga korofa  lakini nyumba ikishakamilika yanaweka uvunguni hayatakiwa hata kuonekana mbele za wageni.

Wasanii wa Tanzania wamekuwa wakitumika kwa stahili hiyo na wengi wamekuwa masikini sana  na hali yao ya uchumi imekuwa ngumu kwa sababu wamekuwa hawathaminiwi tena.

Katika nchi zilizondelea kama Marekani, Uingereza mataifa hayo yanapata mapato makubwa sana kupitia sanaa zao. Takwimu iliyofanywa hapa Tanzania na Lulu Art Promotion inaonyesha kwamba muziki pekee yakee inachangia zaidi ya asilimia moja katika pato la taifa. Naamni wizara ikitumia umakini na ikamamu kuwekeza wasanii wa Tanzania wataweza kuchangia pato kubwa sana katika pato la taifa, lakini pia imesaidia katika kutoa ajira, wasanii wameweza kujiajiri na kuajiri vijana wengi sana.

Mh. Spika katika bajeti ya mwaka 2016/7 serikali ilitenga pesa kidogo sana ambayo ni sh.  bilioni 3 na katika hali ya kustahajabisha ni sh. bilioni 1. 9 ndio ilienda katika wizara hii, na sasa hivi tunaweza kuona imetengwa fedha kidogo ambayo tunaona kama utani. Imetengwa sh. Bilioni 6 katika sekta nzima ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo. Sanaa inatoa ajira kwa vijanaa wengi wa kitanzania tulitakiwa tuweke pesa nyingi na hiyo pesa kufika katika maeneo yanayohusika.

Mh. Spika hivi karibuni kumekuwa na malalamiko ya wasanii wa filamu ambao juzi wameandamana na wakiwa wanapaza sauiti zao wakitaka haki zao za msingi, tunaamini movement yoyote inayofanyika katika kutetea haki inahitaji muungano wa watu wengi. Kama mngetaka kufanikiwa katika hili jambo mngemtumia kama Waziri wa Habari kama alivyofanya press conference yake na Roma tuliona vyombo vyote vikionyesha mshikamano na umoja wao, tunafamu sanaa ya filamu inatoa ajira na sisi tunaitetea.

Kwa mfano mdogo, kabla ya kufanya filamu inabidi utoe sh. 500,000 katika bodi ya filamu kwa ajili ya kupeleka script yako, alafu inabidi utoa tena sh 300,000 kwa ajili ya kupewa kibali cha kushoot, ukishamaliza kushoot, unaipeleka tena kukagulia ambapo unatoa sh. 1,000 kwa kila dakika katika filamu, ukionda kufunguliawa faili Cosota unalipa tena zaidi ya sh. 40,000, baada ya hapo unapeleka TRA wanakupa stika ambayo ni sh. 8 ndani, sh. 8 nje (sh 16. Kwa kila copy), ukimaliza hapo unaenda kunegotiate   na yule distributor ambaye mkishakubalia bei anakata asilimia 30 kwa ajili ya kupeleka kwenye kodi ya Tanzania.

Unaweza kuona jinsi wasanii wa filamu wanavyoumia, lakini njia waliyoitumia kutetea haki zao wametumia mlango mwingine wa kutokea. Kwa hiyo ni muombe waziri huu ni muda wa kukaa na wasanii kuunganisha nguvu zote, tunamuhitaji waziri wa mambo ya ndani, Cosota, Basata ili kujua shida za wasanii  lakini pia tatizo la hati miliki, Mh Spika katika hati miliki namba saba ya mwaka 1999 imeipitwa sana na wakati, wasanii wanaibia kazi zao, uaramia umekuwa mkubwa lakini tukikamata wezi hamnza adhabu kali wanayopata.

Lakini hata juzi msanii Darassa alienda Arusha TRA wakavamia show yake wakasema hayo mapato inabiki wagawane asilimia 18, watu wameituba from nowhere, Darassa amenda Arusha kwa gharama zake, amenda kufanya matangazo, amelipa ukumbi,wameenda wamefunga mageti saa 12 wanamwambia lazima tukate asilimia 18, matokeo yake wamekuja kufungua mageti saa sita usiku, kijana wa watu aliyejiajiri kupitia mzuiki amepata hasara, amepata watu 200/300  TRA wakakata fedha zao.

TRA kama mnataka mapato kaendi chini na wasanii tutengeneze mfumo mzuri ambao utawasaidia wasanii wa Tanzania wanapowekeza kupitia kitu kama hiki

Sasa baada ya hotuba hiyo Rapa Darassa naye akachukua nafasi yake, kupitia mtandao ya instagram Darassa ameandika hivi, “asante sana Mh. Professor Jay kwa kuendelea kupigania sanaa yetu ikae kwenye msingi mzuri japo unajua wewe sio mfanyaji kwa kiasi kikubwa! I can see unataka kue na future nzuri kwa kizazi cha baadae, God bless you brother,”.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad